Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku
tatu kwa wakuu wa wilaya wanaosimamia halmashauri ambazo Mwenge wa Uhuru umekataa
kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyopitiwa na Mwenge huo kutoa
maelezezo ya kina juu ya sababu ya kukataliwa kwa miradi hiyo yenye tamani ya shilingi
1,248,489,871.
“Napenda nitoe
maelekezo kwa Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wenye miradi iliyokataliwa kunipa
taarifa ya kwanini miradi yao haikuzinduliwa/kuwekewa mawe ya msingi. Maelezo
hayo niyapate ndani ya siku tatu kuanzia tarehe ya leo hadi tarehe 14, April,
2019,” Alisisitiza.
Ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru
kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Amos Makalla huku Mwenge huo ukiwa umekimbizwa
katika halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa zikichukua umbali wa kilemeta 832.5 na
kutembelea miradi 35 na vikundi 11 ikiwa na tamani ya shilingi
45,404,104,489.59
Aidha, kutokana na mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kubeba
kauli mbiu isemayo “Maji ni haki ya Kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke
kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa,” hivyo alitoa wito kwa wananachi
kuendela kutunza vyanzo vya maji, kuimarisha jumuia za watumia maji pamoja na
kufanya maandalizi thabiti ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na
kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo.
Kwa upande wake Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019
Ndugu Mzee Mkongea Ali aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kumpa
ushirikiano wa Kutosha tangu wanawasili katika mkoa huo hadi kuondoka na
kuelekea katika mkoa wa Katavi na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa
kufikisha asilimia 55 ya wananchi wa Mkoa huo kupata maji safi na salam.
“Mimi nikupe hongera kwasababu takwimu zinaonyesha katika
mkoa wako wa Rukwa umejitahidi kwa asilimia 55 kuhakikisha wananchi woyte
wanapata maji ya uhakika na salama sambamba na hilo katika kupambana na Rushwa
katika TAKUKURU kuna malalamiko 64 na kesi 59 wanazifanyia kazi, endeleeni
kufanya kazi na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote,” Alisema.
Kutokana na mapungufu yaliyobainika Mwenge wa Uhuru
haukuzindua amakuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitatu, Halmashauri ya
Manispaa ya Sumbawanga mradi mmoja vyumba vitano vya madarasa wenye thamani ya shilingi
76,250,000, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mradi mmoja wa ujenzi wa nyumba
ya waalimu “6 in 1” wenye thamani ya shilingi 174,977,775 na
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mradi mmoja wa maji wenye thamani ya shilingi 997,262,096.
Maelezo ya Picha
IMG_8278
- Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Mzee Mkongea Ali (kushoto)
akitoa pongezi kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa
huo Mh. Joachim Wangabo (kulia) muda mfupi kabla ya Mwenge wa Uhuru
kuelekea Mkoani Katavi tarehe 11.4.2019.
IMG_8294
- Mkuu wa Mko a wa Katavi Mh. Amos Makalla (kulia) akipokea Mwenge wa
Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto)
katika viwanja vya shule ya msingi Milumba Mkoani Katavi.
No comments:
Post a Comment