Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi, akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya kufunga kambi ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface
akieleza namna MOI ilivyojipanga kusogeza huduma kwa wananchi kwa kufanya kambi
za uapasuaji, katika hafla ya kufunga kambi ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na
Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Bugando
Profesa Makubi
akitoa taarifa ya namna kambi ya upasuaji iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya
MOI, Bugando na Cuba ilivyofanikiwa.
Madaktari Bingwa wa MOI, Cuba na Bugando wakifanya upasuaji mkubwa wa mgongo katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mwanza, Tanzania
Zaidi
ya wagonjwa 400 wamehudumiwa kati yao 17 wakifanyiwa upasuaji mkubwa na jopo la
madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Cuba na Bugando katika kambi ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na
Mishipa ya fahamu katika Hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza toka tarehe
8/04/2019 hadi 12/04/2019.
Akihitimisha
kambi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Nyimbi amemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya maboresho
makubwa hapa nchini hususani kwenye huduma za Afya.
"Kambi
hii ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu imewezakana kutokana na
Maboresho yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Tano, kwa niaba ya mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Ndugu John Mongela tunawashukuru wakurugenzi wakuu wa MOI na Bugando
pamoja na madaktari Bingwa wote, kwa hili wananchi wa kanda ya ziwa wamenufaika
sana" Alisema Dkt Nyimbi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema hii ni sehemu ya mkakati wa MOI
na Serikali wa kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi wote
hususani wa mikoa ya pembezoni.
“Baada
ya Serikali kufanya uwekezaji mkubwa MOI ,rufaa za nje ya nchi zimepungua sana
,hivi sasa mpango wa MOI na Serikali ni kuhakikisha huduma za kibingwa
zinawafikia wananchi wote.” Alisema Dkt. Boniface.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Bugando Profesa Abel Makubi ameushukuru Uongozi wa
MOI kwa kukubali kuleta madaktari Bingwa Mwanza ambao wamewahudumia wakazi wa
kanda ya ziwa na kuwapunguzia adha ya kusafiri kwenda Dar es Salaam au nje ya
nchi.
“kwa
niaba ya bodi pamoja na menejimenti ya
Hospitali ya Bugando tunawashukuru wenzetu wa MOI,Cuba kwa kuja kushirikiana
nasi hapa kwenye kambi hii, tunaamini huu ni mwanzo wa ushirikiano baina ya
taasisi zetu wakazi wa kanda ya ziwa wataendelea kunufaika" Alisema
Profesa Makubi.
Taasisi
ya MOI imekuwa ikitekeleza kwa vitendo maagizo ya Serikali ya kuhakikisha
inawaogezea wananchi wa mikoa ya pembezoni huduma za kibingwa ili kuwapunguzia
adha kusafiri kuzifuata huduma hizo MOI.
No comments:
Post a Comment