Viongozi, Wafanyakazi na Wanachama wa Shirika la Under The Same Sun wakiwa katika picha ya Pamoja bungeni Jijini Dodoma leo.
Viongozi, Wafanyakazi na Wanachama wa Shirika la Under The Same Sun wakiwa ndani ya Ukumbi Bunge Jijini Dodoma leo.
Viongozi, Wafanyakazi na Wanachama wa Shirika la Under The Same Sun wakiwa ndani ya Ukumbi Bunge Jijini Dodoma leo.
Shirika la Under The Same Sun lenye kuhudumia na kutetea maslahi ya watu wenye ualbino nchini, linakusudia kufanya semina ya siku moja kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Semina hiyo yenye lengo la kuwapatia uelewa kuhusu ualbino, waheshimiwa wabunge inatarajiwa kufanyika jijini Dodoma kwenye Ukumbi wa Msekwa siku ja jumapili April 14.
Under The Same Sun iliyoanzishwa miaka kumi iliyopita imekuwa ikitoa elimu kwa jamii juu ya ualbino na watu wenye ualbino kwa njia ya mikutano, semina na mafunzo mbalimbali pamoja na kutoa ufadhili wa elimu kwa watu wenye ualbino kuanzia ngazi ya awali, msingi, sekondari hadi chuo kikuu.
No comments:
Post a Comment