Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akimpa pole mjana wa marehemu Clarence
Nanyaro na mtoto wake (kulia) baada ya kuuhifadhi mwili wa marehemu.
Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akimpa pole baba wa marehemu mzee Sabaya
Nanyaro.
Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akiagana na Mkuu wa Boma, Mzee Gadiel
Nanyaro baada ya kumaliza mazishi ya marehemu.
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya
Mpiga Kura, Giveness Aswile wakati watumishi wa Tume walipouaga mwili wa
mtumishi mwenzao Clarence Nanyaro katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto wa marehemu Clarence
Nanyaro (wawili mbele) na mjane wa merehemu (kushoto aliyeshika kichwa) wakiwa
kwenye majonzi wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mpendwa wao.
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi an waombelezaji wengine wakishiriki katika ibada ya kumuaga
marehemu Clarence Nanyaro katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mjane wa Marehemu Clarence Nanyaro
akiaga mwili wa marehemu.
Baba wa marehemu mzee Sabaya Nanyaro
akiaga mwili wa marehemu mwanaye wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu.
Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
marehemu.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki
wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Baba na mama wa marehemu wakiwa an
nyuso za huzuni wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu.
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria
kumuaga marehemu Clarence Nanyaro, kwenye kijiji cha Nkomaala wilayani Meru
mkoani Arusha.
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria
kumuaga marehemu Clarence Nanyaro, kwenye kijiji cha Nkomaala wilayani Meru
mkoani Arusha.
Baadhi ya waombolezaji wakishusha
mwili wa marehemu kwenye kaburi lake.
Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akiweka shada la maua kwenye kaburi la
marehemu Clarence Nanyaro, aliyezikwa mwishoni mwa juma hili kijijini kwao
Nkomaala, wilayani Meru mkoa wa Arusha. Picha na NEC.
Na Mwandishi Wetu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeungana familia,
ndugu, jamaa na marafiki kuuaga na kuuhifadhi
kwenye makazi yake ya milele, mwili wa
mtumishi wake Clarence Nanyaro aliyefariki Aprili 2 mwaka huu na kuzikwa
kijijini kwao Nkomaala, wilayani Meru mkoani Arusha.
Tume katika mazinshi hayo iliwakilishwa
na Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe
aliyeambatana na baadhi ya watumishi kumhifahdi marehemu Nanyaro aliyekuwa
Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Habari wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura.
Akizungumza wakati akitoa salamu za
rambirambi, Mkurugenzi Wandwe alisema Tume inaungana na familia, ndugu, jamaa
na marafiki kuombeleza msiba wa mtumishi wake kwani marehemu Nanyaro alikuwa
mtu wa kuaminiwa kutokana na utendaji kazi wake mzuri.
“Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi napenda
kuwasilisha salamu za rambirambi kwa masikitiko makubwa.Marehemu alifanya kazi
vizuri sana na tulimuamini na kumpenda, lakini kwa mapenzi ya Mungu amemchukua, tunasema Bwana alitoa na
Bwana ametwaa, Jina lake lihimidewe” alisema Mkurugenzi Wandwe na kuongeza
kuwa.
“Kuhusiana na suala la rambirambi
napenda kueleza kwamba Ofisi inafanya utaratibu wa michango mbalimbali ambayo baada ya hapa tutawasiliana na familia kujua
utaratubu wa kuwasilisha.”
“Pili kwa kuwa marehemu alikuwa
mtumishi wa Serikali, kwa niaba ya Tume niseme kwamba zitafanyika taratibu za
kisheria, kanuni na taratibu kuhusiana na stahiki zake na atapewa mtu kama
sheria zinavyoelekeza”.
Akitoa shukrani kwa niaba ya familia,
Mkuu wa Boma Mzee Gadiel Nanyaro aliishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa
huduma waliyoitoa kwa marehemu na kumuomba mwakilishi wake kufikisha shukrani
hizo ofisini kutokana na ushirikiano mkubwa waliyoutoa kwa familia.
Marehemu Nanyaro mbali na kufanya kazi
Tume tangu mwaka 2015 hadi umauti unamkuta, pia alifanya kazi Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Ofisi ya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Utangazaji
(TBC) kwa nafasi mbalimbali.
Alifariki tarehe 2 Aprili mwaka huu kutokana
na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na hivi karibuni alipata ‘Mild Stroke’
ambao ulisababisha alazwe kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa takribani
siku 19 hadi umauti ulivyomkuta.
Akisoma akitoa salamu za rambirambi
wakati watumishi wa Tume wakiaga mwili wa marehemu jijini Dar es Salaam,
Mkugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya NEC, Giveness Aswile alisema
alitoa shukrani za Tume kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
na Hospitali ya Bochi kwa jitihada walizofanya katika kuokoa uhai wa marehemu.
“Tume inatoa shukrani kwa madaktari na
wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bochi kwa jitihada
walizofanya katika kuokoa uhai wa marehemu.Pia inawashukuru viongozi wa dini,
watu binafsi na taasisi mbalimbali kwa kumuhudumia marehemu wakati wa uhai
wake.” alisema Mkurugenzi Aswile.
Marehemu ameacha mjane na watoto.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la
Bwana lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment