Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mfano hundi ya Shilingi Milioni moja, Failuna Mgata, ambaye amekua mshindi wa mbio za kilometa 21 kwa wanawake wakati wa mbio za Sokoine Memorial Marathon zilizofanyika, mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Kushoto ni Mjane wa Marehemu Edward Sokoine. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka
vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali
kuendelea kuviendeleza kwakua Michezo katika Dunia ya leo ni ajira.
Mhe.Waziri
Mkuu ameyasema hayo Aprili 06,2019 Jijini Arusha katika Mashindano ya Riadha ya
Sokoine Memorial Marathon yaliyolenga kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani Hayati
Edward Moringe Sokoine aliefariki miaka 35 iliyopita ambapo ameeleza kuwa
marehemu Sokoine alikua anapenda sana michezo pamoja na kufanya kazi kwa bidii.
“Michezo
ni muhimu kwakua inaleta umoja,ushirikiano furaha lakini zaidi katika dunia ya
leo ni ajira ya kuaminika hivyo ni lazima vijana mkatumia vipaji mlivyonavyo
katika michezo mbalimbali ili muweze
kupata ajira na hatimaye mfanikiwe kama wengine waliofanikiwa kupitia
sekta hii”.alisema Mhe.Kassim Majaliwa.
Aliongeza
kuwa Michezo kwa sasa inatangaza Taifa letu ambapo ametolea mfano wa Timu ya
Taifa (Taifa Stars) ambayo hivi karibuni imefuzu kushiriki Michuano ya AFCON itakayochezwa
baadae mwezi juni huko nchini Misri,Timu ya Vijana chini ya Miaka 17 “Serengeti
Boys” itakayoshiriki Mashindano hayo ambayo yatafanyika hapa nchini kuanzia
April 14 -28 mwaka huu ambapo timu hiyo inatakiwa kushinda mechi mbili tuu ili
iweze kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Brazili.
Katika
hatua nyingine Mhe.Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kumuenzi
Hayat Edward Moringe Sokoine kutokana na mchango wake wa kuletea Taifa
maendeleo kwa kuhimiza wananchi kujituma, kuwa wazalendo pamoja na kudumisha
amani ya nchi.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
amesema kuwa mchezo wa riadha umeendelea kufanya vizuri kimataifa kwakua nchi
imepata wawakilishi watakaoshiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa
kufanyika mwaka 2020 huko Tokyo Japan,mashindano ya riadha ya Dunia pamoja na
Jumuiya ya Madola.
Mhe.Shonza
ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Chama cha Riadha nchini inaendelea na
maandalizi ya mashindano ya riadha ya kimataifa ya All Africa Games,World
Championship na African Cross Country Championship ambayo Tanzania ndio itakuwa
Mwenyeji.
“Mchezo
huu wa riadha umeitangaza vyema nchi yetu kupitia wanariadha mbalimbali
waliofanya vizuri kimataifa ambapo timu yetu ya Taifa ya mbio za nyika
ilishiriki mashindano nchini Dernmark na kumaliza katika nafasi ya 8,10 na 11
kupitia wanariadha Failuna Matanga,Emmanuel Ginik,Gabriel Geay na Aliphonce
Simbu”.alisema Mhe.Shonza.
Hata hivyo
Rais wa Chama cha Riadha nchini
Mhe.Antony Mtaka amewataka waandaaji wa mbio mbalimbali nchini kuzingatia
Sheria na taratibu hususan usajili wa
mbio hizo katika Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) kabla ya kuzitangaza ama kuhamasisha wadau na wananchi kushiriki.
Naye
mshindi wa mbio za Kilometa 21 kwa wanawake Bibi Failuna Matanga amesema kuwa
mafaniko anayopata kupitia riadha ni kutokana na kujituma kufanya mazoezi
pamoja na nidhamu katika mchezo huo.
Mbio hizo
za Soikone Memorial Marathon zilishirikisha mbio za Kilometa 2 na nusu,Kilometa
05 na kilometa 21 ambapo Watoto,wasichana
na wavulana walishiriki na washindi kupewa zawadi ikwemo pesa pamoja na medali.
No comments:
Post a Comment