Na
Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Jamii
yatakiwa kutomaliza masuala ya ukatili wa kijinsia ndani ya familia na badala
yake ishirikiane na Serikali ili sheria ichukue mkondo wake.
Hayo
yameelezwa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali
la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Zainab Mussa Bakar kuhusu lini Serikali italeta
muswada wa sheria bungeni ili kurekebisha sheria hiyo iwe kali zaidi.
"Kwa
ujumla sheria zilizopo zinajitosheleza kabisa kuwashughulikia wale wote wanaokutwa
na hatia katika makosa ya ubakaji, kunajisi watoto wa kiume na wa kike. Sheria
ya Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,
imeelekeza adhabu kali kwa yeyote atakayebainika kutenda kosa la kumdhalilisha
mtoto au kumbaka ikiwemo kifungo cha miaka 30," amesema Dkt. Ndugulile.
Ameendelea
kusema kuwa, imekuwa vigumu kuwatia hatiani wakosaji hasa wa ndani ya familia
kwa kukosekana kwa ushahidi ikizingatiwa matukio mengi hufanywa na watu walio
karibu na familia ambapo wengi wao wanaogopa kutoa ushahidi kutokana na hofu ya
kupoteza mmoja ya wanafamilia kutokana na adhabu ya kifungo cha maisha.
Aidha,
kutokana na mtazamo hasi wa jamii, familia nyingi uhofia kudhalilika au
kunyanyapaliwa baada ya kubainika mkosaji.
Hata
hivyo, Serikali inajitahidi kuweka mikakati ya kusaidia kupunguza au kumaliza
kabisa tatizo hilo, lakini familia nyingi zimekuwa hazitoi ushirikiano ili
kuwatia hatiani wale wanaopatikana na makosa ya ukatili wa kijinsia ndani ya
familia.
No comments:
Post a Comment