Kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo akiwa mbele ya waandishi wa habari akielezea lengo la kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo ili kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakiwasikiliza viongozi wa timu ya Lipuli fc juu ya mipango na mikakati ya Harambee ya kuichangia timu hiyo.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
UONGOZI wa timu ya soka inayoshiliki Ligi Kuu
Tanzania Bara, Lipuli FC ya
mkoani Iringa umepanga kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo kwa lengo la kuimarisha
uchumi kutatua changamoto za mishahara pamoja ada za wachezaji ambazo hadi hii
leo bado wanadaiwa na wachezaji wa klabu hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoa Iringa kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo
alisema kuwa lengo la kuitisha harambee hiyo ni kufanikisha kupata fedha za
kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na
wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu
Tanzania bara.
“Ni
kweli hatujalipa wachezaji miezi miwili hadi hivi sasa na bado tunadaiwa pesa
za usajili kwa wachezaji wetu hiyo tumeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuinusu
timu kwa msimu ujao kuondokewa na wachezaji wetu ambao ni wazuri kweli kweli na
wanaujua mpira sana” alisema Kihwelo
Kihwelo
aliongeza kuwa harambee hiyo itafanyika siku ya jumapili tarehe 7 / 4 / 2019
siku ya jumapili katika ukumbi wa kichangani uliopo manispaa ya Iringa ambapo
wanatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda kuwa
mgeni Rasmi
“Siku
ya harambee hii tunatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda kuwa
mgeni Rasmi akiambatana na wadau mbalimbali akiwepo mkuu wa mkoa wa Iringa
pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huu ambao tunategemea watachangia timu
yao ambayo inafanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara” alisema Kihwelo
Kihwelo alisema wanatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni
miatatu kwenye Harambee hiyo ambazo zitasaidia kuendesha timu bila kuwa na deni
lolote kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo na kuweza kupata usajili mpya wa msimu
ujao wa ligi kuu Tanzania Bara
“Tunalipa
zaidi ya milioni ishirini na nne kila mwezi kwa ajili ya mishahara tu ya
wachezaji wa timu na tunagharamia zaidi ya laki tatu kwa siku kwa ajili ya
kambi ya timu hivyo utaona kwa namna gani timu inavyogharimu kiasi kikubwa cha
fedha na timu hadi hivi sasa haina mdhamini yeyeote yule” alisema Kihwelo
Aliezea
kuwa mikakati ya msimu ujao ni kuhakikisha timu inapata mdhamini wa kudumu kwa
kuwa timu yetu ya Lipuli imekuwa ikipata matokeo mazuri kila msimu hivyo
itatusaidia kupata mdhamini ambaye ataamini kuwa timu hiyo inauwezo wa
kuitangazia bidhaa yake.
Kwa upande
wake katibu mkuu wa klabu hiyo ya Lipuli Julius Leo ameomba wananchi,wadau wa
soka na wapenzi wa klabu ya Lipuli kuichangia timu hiyo kwa kutumia akaunti ya benk
ya CRDB 01J2072252000 na kwenye namba ya
simu ya MPESA ya timu hiyo ambayo ni 0744 16 24 46 inayojulikana kwa jina la
LIPULI FC
No comments:
Post a Comment