Mhandisi kutoka Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha
ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Joyce Mbunju, akielekeza jambo
kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiteto, mkoani Manyara, kuhusu umuhimu wa
masomo ya Sayansi na Hisabati.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Dirma, mkoani Manyara, wakimsikiliza Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake
katika kazi za barabara, Judith Aron (hayupo pichani), alipofika shuleni hapo
kuhamasisha umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Wahandisi kutoka Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha
ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakigawa zawadi za
madaftari na kalamu kwa mwanafunzi Esther Paschal wa Shule ya Sekondari Dirma,
mkoani Manyara, aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
Wahandisi wanawake
kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo
maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakiwa katika
picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Babati, mkoani
Manyara, mara baada ya kutoa elimu ya umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati
kwa wanafunzi hao.
Picha
na WUUM.
No comments:
Post a Comment