Katibu
Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, akizungumzia ujioa wa timu ya Sevilla ya Hispania itakayocheza na Simba Mei 23, 2019 kwenye Uwanja wa Taifa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania “TFF” limetangaza
timu ya Simba ya Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na
Sevilla ya Hispania Mei 23,2019 Uwanja wa Taifa.
Klabu
ya Simba imetajwa kucheza mchezo huo dhidi ya Sevilla kwa kigezo cha
Klabu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa Cup
kwa timu zinazodhaminiwa na SportPesa.
Sevilla waliopo kwenye Ligi Kuu ya Hispania La Liga wataingia Tanzania Mei 21,2019 tayari kwa mchezo huo.
Katibu
Mkuu wa TFF Kidao Wilfred amesema kigezo kikubwa kilichotumika kuchagua
timu ya kucheza mchezo huo ni timu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika
mashindano ya SportPesa ambapo Simba ilifikia hatua ya nusu fainali.
Amesema ratiba ya Ligi Kuu imebana kimetumika kigezo cha mashindano ya SportPesa kumpata muwakilshi wa kucheza na Sevilla.
Mkurugenzi
wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tarimba Abas awali kulikuwa na wazo
la kuzikutanisha Simba na Young Africans ili kupatikana timu moja
lakini ratiba imekuwa ngumu kuzikutanisha timu hizo au kuchezwa michezo
mawili.
Ameongeza kuwa kigezo cha kutumia mashindano ya SportPesa kinaondoa ugumu wa kupatikana timu ya kucheza na Sevilla.
Tayari maandalizi kwaajili ya mchezo huo yanaendelea.
No comments:
Post a Comment