Mvua kubwa iliyonyesha mkoani Arusha imesababisha kuharibika kwa miundombinu ya barabara kama picha inavyoonyesha. (Picha na Grace Macha).
NA GRACE MACHA, ARUSHA
MVUA kubwa iliyonyesha kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa
Arusha imesababisha madhara makubwa ikiwemo kuharibu miundombinu ya
barabara, kunusurika kufa baada ya nyumba kadhaa kuja maji na kuta
kuanguka.
Mvua hiyo ilinyesha usiku wa juzi kuamkia jana ambapo
kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha barabara zilijaa maji
yaliyokuwa yakipita juu ya barabara.
Aidha, masiliano yalikatika kwa muda maeneo ya King'ori
kwenye barabara kuu ya Arusha - Moshi baada ya kipande cha barabara
kuharibiwa na maji ya mvua.
Kwenye baadhi ya barabara za jiji magari yalizuiwa kupita kutokana na maji ya mvua kupita juu ha barabara.
Wakazi wa kata mbalimbali za jiji la Arusha na wilaya ya
Arumeru walionekana wakiwa kwenyw hekaheka za kuzibua mitato ya maji na
wengine wakitiboa kuta za nyumba zao kuruhusu maji ya mvua kupita.
Kata zilizopata madhara ni pamoja na Osunyai Jr, Unga LTD,
Kimandolu,Engutoto, Moshono na Kiranyi ambapo baadhi ya wakazi
wamelazimika kuhama nyumba zao kutokana na kujaa maji.
Meneja wa Wakala wa barabara Tanzani (Tanroads), Mkoani
Arusha, Mhandisi, John Kalupale, alithibitisha maji ya mvua kusababisha
madhara makubwa ya uharibifu wa miundombinu ya barabara kwenye baadhi ya
barabara wanazozihudumia.
“Barabara ya Arusha kwenda Moshi eneo la King’ori
imevunjika na magari madogo yalizuiliwa kwa muda, lakini barabara
zilizoharibika utaratibu wa kuzikarabati umeshaanza,”alisema Kalipale.
Kalupale alisema kuwa wataalam wa Tanrods wako wanatembelea
na kukagua barabara zote zilizoathirika ili kutambua ukubwa wa tatizo.
“Tutatembelea barabara zote kuangalia ukubwa wa madhara
yaliyosababishwa na mvua hii na baada ya hapo tutatoa taarifa
kamili,”alisema Kalupale.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan
Shana alipotafutwa kwa njia ya simu alipokea msaidizi wake na kusema
kuwa kiongozi huyo yuko kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.
Hata hivyo RPC Shana alionekana akipita maeneo mbalimbali
ya jiji la Arusha ambapo msaidizi wake mmoja alionekana alionekana
akimuokoakijana mmoja aliyekuwa akisombwa na maji.
No comments:
Post a Comment