Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa huduma ya WhatsApp kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake. (Picha na Francis Dande).
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Tigo Tanzania, jana ilizindua huduma ya whatsApp kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake.
Huduma
hii ya kidijitali, itawawezesha wateja wa Tigo kutuma dukuduku zao na
kupokea majibu ya papo kwa papo watakapotumia namba ya WhatsApp ambayo
ni 0675100100.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam jana, Mkuu
wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola alisema,
Tigo imekuwa kampuni ya kwanza nchini kutumia mtandao wa kijamii wa
WhatsApp kuwahudumia wateja wake.
“Kupitia
huduma hii mpya, wateja wa Tigo watapata uzoefu binafsi pamoja na
kupata majibu ya papo kwa papo watapotaka kupata ufafanuzi wa jambo au
utatuzi wa changamoto zozote katika kutuia mtandao wetu,” alisema
WhatsApp
ni moja kati ya mitandao ya kijamii yenye nguvu sana duniani kwa sasa.
“Kwa kuzingatia ukweli huu, huduma hii itawawezesha wateja wa Tigo
kupata huduma binafsi na zenye usalama.
Alisema
uzinduzi wa huduma hiyo ni moja kati ya mikakati yao ya kuhamasisha
maisha ya kidijitali, pia kupanua wigo wa namna wateja wanavyoweza
kuhudumiwa tunavyoongeza WhatsApp kwenye huduma zao za mitandaoa ya
kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter.
Alisema
huduma ya WhatsApp inapitakana kwa wateja wote wa Tigo na kwamba huduma
hiyo imetengenezwa maalum kwa ajili ya kumhudumia mtu mmoja mmoja na
siyo kuwahudumai watu kwa pamoja kama kundi (group la WhatsApp).
“Mteja
siyo tu ataweza kujielezea kupitia huduma hii lakini pia anaweza kutuma
picha kwenye mfumo wa ‘screenshot’ kwenda namba 0675100100 na atapata
majibu ya papo kwa papo kwa kile atachoakiuliza au kutaka
ufafanunuzi/utatuzi,” alisema.
“Tigo
Tanzania inajivunia kuwa kampuni ya simu namba moja kwenye mageuzi ya
kidijitali pamoja na uvumbuzi. Tigo imeweza kuwa ya kwanza kuzindua
bidhaa nyingi kwenye soko la Tanzania ambazo zinathibitisha dhamira yetu
ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu pamoja na uzoefu wa aina yake.
huduma hii ya WhatsApp ni sehemu ya safari yetu hii ya mageuzi ya
kidijitali,” aliongeza.
Wateja
wanaotumia WhatsApp wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa
wateja cha Tigo muda wowote wanaopenda na kama itatokea kukawa na
kuchelewa kupata mrejesho atapokea ujumbe mfupi.
Alisema
huduma hiyo mpya ya WhatsApp kwa ajili ya kuwahuduma wateja, ni sehemu
ya mkakati wa kampuni ya Tigo kuwapatia wateja wake uzoefu wa aina yake
na wa kipekee wa huduma zake kwa njia ya kidijitali na kurahisisha
maisha yao ya kila siku kupitia huduma zilizojaa ubunifu.
No comments:
Post a Comment