Na Mauwa Mohammed Zanzibar
Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka Chama cha Wandishi wa habari wanawake Tanznania TAMWA wameiomba Serikali ya Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika kisiwa cha Tumbatu hasa masuala ya udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Hayo wameyabainisha wakati wa kikao cha Kutathimini mradi wa malezi mbadala Unaotekelezwa katika kisiwa cha Tumbatu chini ya ufadhili wa kijiji cha Malezi S.O.S na TAMWA kwa ufadahili wa washirika wa maendeleo chini Dermark.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar Mratibu wa Mradi huo Mariam Ame alisema licha ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi za kiraia lakini bado kumeonekana kuwepo kwa mfumo dume unaosababisha watoto kukosa haki zao za msingi.
Mratibu huyo alisema hali hiyo imeonekana hukosekana malezi ya pamoja ya baba na mama jambo ambalo linapelekea viashiria vya hatari ya kukumbana na masuala ya udhalilishaji.
Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa katika utekelezaji wa Mradi huo katika kisiwa cha Tumbatu ni kuendelea kwa maswala ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ambayo hadi sasa wakazi wa kisiwa hicho wamekuwa na muhali katika kuyaripoti matukio hayo.
Alisema kwa mujibu wa Katibu Tawala wa Wilaya Ndogo ya Tumbatu kuna kesi nyingi ambazo hazijaripotiwa kutokana na Tabia ya wananchi wengi kujadili na kusuluhishana wenyewe kwa wenyewe.
Alisema Tumbatu kunahitajika kutolewa elimu juu maswala ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo jamii hiyo kujua athari zinazotokana na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto.
Aidha kwa Upande wake mratibu wa malezi mbadala kutoka katika Vijiji vya kulelea watoto yatima SOS Nyezuma Simai Issa amesema Mradi huo unalengo la kuwapa malezi bora kwa watoto ambao wamepoteza mzazi mmoja pamoja na familia ambazo zinaisha katika mazingira magumu.
Amesema Mradi huo ambao unatekeleza mambo matatu ikiwemo kuwajengea uwezo wadau kuhakikisha kwamba lengo la mradi la malezi mbadala linafanikiwa Miongoni mwa wadau hao ni asasi za kirai, masheha, pamoja na maafisa kutoka serikalini.
Aidha amesema mradi huo pia ulitenga fungu dogo katika kuboresha huduma za malezi ikiwemo elimu, Afya, na kuwapatia jamii mtaji ili kuendesha maisha yao na kulea familia zao.
Jumla ya familia 50 katika kisiwa cha Tumbatu zimefaidika na Mradi huo wa malezi mbadala ikiwemo watoto wa kike 29 na wakiume 21 wakiwa chini ya walezi 31.
Mradi huo wa malezi mbadala unateekelezwa katika nchi 3 za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda, Tanzania/ Zanzibar na unaotekelezwa katika kijiji cha SOS Zanzibar kwa kushirikiana na asasi za kirai kama vile TAMWA, MUZDALIFA, na kufadhiliwa na SOS Denmark.
No comments:
Post a Comment