Madaktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
kushirikiana na mwenzao wa Hospitali ya
Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic
Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri.
Kambi hiyo ni
maalum kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa
wenye matatizo hayo ambao bila ya kupata mtaalamu mwenye ujuzi wa hali ya juu
wa kuzibua mishipa hiyo wangefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.
Matibabu hayo
yanafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambapo mgonjwa anatobolewa tundu dogo
katika paja ambalo linapitishwa vifaa maalum vya kuzibua mishipa ya damu ya
moyo (Stent).
Katika kambi
hiyo wataalamu wa afya wa JKCI watapata elimu ya jinsi ya kuzibua mishipa ya
damu ya moyo ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa.
Jumla ya
wagonjwa 15 ambao mishipa yao ya damu mmoja hadi mitatu imeziba wanatarajiwa
kutibiwa katika kambi hiyo iliyoanza leo
tarehe 23 hadi 25/4/2019. Hadi sasa
wagonjwa watano wameshatibiwa na hali zao zinaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment