Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai (kushoto), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika na Naibu wake, Dk. Mary Mwanjwelwa, wakisikiliza mada ya Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark tawi la Tanzania, John Ulanga, kwenye semina ya wabunge wanachama wa Chama cha Wabunge Wanaopambana Rushwa (APNAC) walipokuwa wakijadili kuhusiana na maendeleo ya biashara nchini, iliyofanyika jijini Dodoma hivi karibuni. (Na Mpiga Picha Wetu).
Dodoma, Tanzania
Serikali ya Tanzania Awamu ya Tano chini ya Dk. John
Pombe Joseph Magufuli, imedhamiria kwa dhati, kuendelea kuboresha mazingira ya
uwekezaji nchini na mazingira ya kufanya
biashara Tanzania, hivyo kuipongeza Taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA), kwa kufadhili miradi ya kuboresha biashara
kwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa na ufadhili wake katika miradi ujenzi wa
mifumo ya kidigitali ya kufanya biashara, hivyo kuongeza ushindani wa Tanzania
katika kufanya biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kimataifa.
Pongezi hizo, zimetolewa na Waziri wa Viwanda na
Biashara, Mhe. Joseph Kakunda, katika
semina ya Wabunge Kuhusu Fursa za
Biashara Ukanda wa Afrika Mashariki,
liyofanyika jana, katika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma na ambapo TradeMark East Afrika, iliwasilisha Mada ya Mchango wake
katika Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini, Tanzania.
Waziri Kakunda, amesema Trade Mark East Africa,
wanafanya kazi nzuri sana kuisaidia
serikali, ujenzi wa miundombinu ya kisasa na kuboresha mifumo ya kiundeji
kuboresha kufanya biashara, biashara ikiwa nzuri, uchumi utakuwa mzuri na TRA
itakusanya kodi zaidi na kuleta maendeleo kwa taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejment ya Utumishi
wa Umma, Mhe. George Mkuchika, amesema semina hiyo ya TradeMark kwa Wabunge,
imewafungua macho kuhusiana na vikwazo vya kisera, kimiondombinu na kisheria
vinavyokwamisha biashara, hivyo Wabunge kama watunga sheria, ni muhimu
wakavielewa ili kushinikiza mabadiliko ya sheria, taratibu na kanuni za kuodoa
vikwazo vyote vya kibiashara na kuifanya Tanzania, kuwa ni nchi kivutio kwa
uwekezaji na kufanya biashara.
Kwa upande wake , Mkurugenzi Mkaazi wa TradeMark
East Africa, Tawi la Tanzania, John Ulanga, amesema Tanzania ndio nchi yenye
fursa kubwa zaidi kibiashara kuliko nchi nyingine zote, kufuatia kupakana na
nchi 6 ambazo hazina bahari, hivyo Tanzania ina fursa ya kuwa nchi kitovu cha
Biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.
Semina hiyo pia ilipokea
mada mchango wa TradeMark East Africa
kutoka TRA, TFDA, TPA na Wizara mbalimbali.
No comments:
Post a Comment