HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 30, 2019

WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment

Pages