Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
kupitia Ndaki, Shule Kuu na Tasisi zake imeonesha tafiti zilizofanywa na
wanataaluma, pamoja na wanafunzi wake ili tafiti hizo zitumike kutatua
changamoto zilizopo nchini hususani katika suala zima la maendeleo.
Tafiti hizo ambazo zimeoneshwa
katika Kampasi ya Mwalimu Nyerere, Chuo kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam
(DUCE), Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) pamoja na
Ndaki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT) zimefanyika kwa siku mbili
kuanzia tarehe 3 na 4 Aprili 2019.
Katika maonesho hayo, wadau na
wanafunzi kwa ujumla wametembelea mabanda na kujifunza masuala mbalimbali kutoka
kwa wahadhiri na wanafunzi wa shahada za awali na zile za juu.
Kauli mbiu ya wiki ya Tano ya
Tafiti hizo Ni “Utafiti kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu” inatarajia
kukamilika Tarehe 6 hadi 8 Mei, 2019 kwa maonesho ya jumla ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu Tafiti na
Maarifa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Cuthbert Kimambo (mwenye Tai)
akiwa na Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji Dkt. Pendo Balangwa wakipokea
maaelezo kutoka kwa wataalamu wa Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (COET) walipotembelea
banda lao Katika Kampasi ya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu Tafiti na
Maarifa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Cuthbert Kimambo (mwenye Tai)
akiwa na Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji Dkt. Pendo Balangwa wakiangalia na
kupokea maelezo ya mtambo wa kupoza hewa kutokwa kwa mmoja wa wanafunzi wa
shahada ya juu katika Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (COET) katika wiki ya
Tafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment