HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2019

Ukiwekeza, usiyaweke mayai yote kapu moja

Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS PLC, Bi. Martha Mashiku, akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wastaafu watarajiwa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Ukumbi wa Mkutano wa Hoteli ya Kings Way, mkoani Morogoro. 

 Semina ya ikiendelea mkoani Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa semina ya wastaafu iliyoandaliwa na Shirika la Tija la Taifa 'National Institute of Productivity' wakisikiliza mada juu ya uwekezaji wa pamoja pindi watakapostaafu.
Ofisa Mafunzo kutoka Idara ya Uendeshaji UTT AMIS, Abbas Kandila (kulia), akiwaeleleza jinsi ya kujaza fomu za kujiunga Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja baadhi ya wanachama wa Kampuni ya Ushauri  Kibiashara ya Namaingo Business Agency wakijaza fomu.


NA MWANDISHI WETU

UMEWAHI kujiuliza nini tofauti yakuwekeza kwaatika kama katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa UTT AMIS na kuweka fedha yako benki ama katika kibubu?

Swali hili ni muhimu kwa sababu hivi ni vitu viwili tofauti, japo fedha ndio inahusika.

Wakati kuwekeza fedha ni njia ya kufanya fedha zako ziweze kuzaa nyingine, kwingineko kwa mfano katika benki, ni kwa ajili ya usalama.

Kimsingi, ili uweze kuwekeza, unahitaji uwe na chanzo kingine cha mapato.

Aidha, utaweza kuwekeza iwapo tu utakuwa na akiba ya kutosha uliyojiwekea kutoka katika chanzo chako chako cha mapato.

Kwa upande wa akiba, ni sehemu ya fedha uliyohifadhi kutoka katika chanzo chako cha mapato.

Chanzo hiki chaweza kuwa biashara, kazi na na kadhilika. Akiba hii hupatikana pale tu unapokuwa na nidhamu ya matumizi.

Katika mahojiano na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, anasema jambo la msingi hapa ni kutambua katika kuwekeza, kuna hali ya kupata na kukosa.

Anasema, kupata huendana na mambo mengi ikiwemo hali ya uchumi wa nchi, hali ya siasa ya nchi, uweledi wa mwekezaji, nguvu ya soko, uwepo wa wateja, ubora wa bidhaa au huduma na hali hatarishi na mabo mengine.

Kwamba, kutokana ukweli mazingira ya Uwekezaji yana kabiliwa na dhoruba ambazo zaweza kuwa kubwa au za wastani; wakati mwingine dhoruba huwa hazipo kabisa.

“Wewe kama mwekezaji unayo kazi kuu moja ya kuhakikisha kuwa unaifikisha meli (Uwekezaji wako) salama kule unapotaka ufike.

“Vinginevyo Uwekezaji kama meli unaweza ukishia pasipo julikana baharini. Ili chombo kisizame shurti ujue unatoka wapi na unakwenda wapi na njia utakazo pita na changamoto zake, uwe umezitafiti na kuchukuwa tahadahari kabla ya safari.

“Yaani, wakati wa safari ukutane na yale ambayo hata ungefanya vipi usinge juwa kama yata tokea,” anasema Mbaga.

Kwa hiyo, Mbaga anasema kila kampuni ni lazima iwe na utaratibu wa kukabiliana na athari zinazoweza kutokea katika Uwekezaji kwa mfano katika Uwekezaji wa pamoja meneja ni lazima awekeze katika maeneo zaidi ya moja.

“ Yaani inapaswa akwepe kuweka katika kapu moja, hii ina maana ya kuwa kapu moja likidondoka mengine yanakuwa yamesimama, pia athari zinapunguzwa kwa kutumia utaalamu kwa maana ya kuwa ni lazima afanye upembuzi wa kitaalamu kabla ya kuchaguwa ni wapi awekeze.

“Kwa mfano, kama anakopesha uwezo wa aliyekopeshwa kulipa upo? Historia yake dhidi ya madeni ukoje?; Pia anaangalia mfumuko wa bei je kwa kuzingitatia utaalamu thamani ya fedha inatarajiwa kuwa vipi?; anafanya tathimini ya hali ya uchumi na siasa ya sasa na ya baadae ; na mambo mengine kadha wa kadha.

Mbaga anasema uwekezaji unaochukuwa tahadhari dhidi ya dhoruba na majanga kabla ya kutokea na kuweka hatua zipi za kuchukuwa kama hali hatarishi ikitokea.

“Ukiwa ameangalia tahadhari zote kabla, utakuwa umejiweka vizuri katika kutia wawekezaji imani kuwa hata wakati wa mawimbi mambo yatakuwa mazuri.

“Tukichukuwa tahadhari kabla itasaidia katika maamuzi kwa mfano lipi lianze kwanza na lipi lingojee, tuwekeze fedha zetu vipi?

“Na itatusaidia kutotoka sana njee ya njia kuu ya kutufikisha katika mpango wetu huku tukitumia gharama ndogo kukabiliana na tahadhari kama itatokea,” anasema Mbaga.

Sehemu muhimu za kuangalia mianya ya athari katika Uwekezaji ni kama kwenye: Mpango mkakati-Kuingia kwa mshindani sokoni; Fedha-ongezeko la riba katika mikopo; matakwa ya Uwekezaji-kanuni mpya katika Uwekezaji.

Nyingine ni Utendaji-Uchovu au mitambo kuharibika, Menejimenti- yaweza kuwa mbovu au badilika; Mazingira; Uchumi, Siasa na kadhalika.

Kama umechukuwa hatua kabla, janga likitokea unaweza libeba sababu gharama za kuliondoa ni kubwa sana, pia waweza kuhamisha tahadhari nah ii ni kwa kutumia bima, na wakati mwingine utapaswa kubadili mfumo mzima wa jinsi unafanya jambo fulani. Cha muhimu uwe na sera juu ya majanga.

Kwa hiyo kiujumla tunaweza sema kuwa tahadhari katika Uwekezaji wa pamoja ni kama zile za kwenye Uwekezaji mwingine kwa mfano pesa za mfuko katika Uwekezaji zinakopeshwa kwa riba, riba inapanda na kushuko kutokana na mwenendo wa soko la fedha.

Anasema, riba ikishuka ina maana faida kwa mkopeshaji inapungua. Pia riba ikishuka thamani ya Uwekezaji inaweza pungua.

“Pia mojawapo ya sehemu mifuko inawekeza ni kwenye kukopesha, ukikopesha aliyekopeshwa anaweza shindwa kulipa bahati nzuri UTT AMIS haikopeshi watu au taasisi binafsi, hukopesha serekali tu kupitia hati fungani,” anasema na kuongeza:

“Mabenki kupitia akaunti za mda maalumu na pengine madeni kwa benki ya muda mfupi. Tahadhari nyingine ni Uwekezaji katika hisa, hisa zina tabia ya kupanda na kushuka, japo hisa ndiyo chachu ya faida wakati mwingine zinashuka na aidha kupunguza faida au kuleta hasara.

“Kumbuka, tukiongelea athari, mfano uchumi ukianguka haijalishi hela zako ziko wapi lazima kwa namna moja au nyingine utaguswa.

“Lakini uzuri wa Uwekezaji wa pamoja ni kwamba meneja (UTT AMIS) ana wekeza sehemu nyingi hivyo basi kupunguza wastani wa mtikisiko wakati mambo hayaendi sawa na pia kuongeza faida wakati mambo yanakwenda vizuri,” anasisitiza Mbaga.

Anasema jambo jingine la kukumbuka, ni kuwa meneja akiwekeza kwenye hisa, au ukawepo mfuko ambao unawekeza katika masoko ya hisa tu, basi tunasema kuna nafasi kubwa ya kupata faida, lakinipia tahadahri ni kubwa sana, na mara nyingi Uwekezaji wa sehemu hii unahitaji muda mrefu.

Haya hivyo, anasema meneja anayewekeza katika hati fungani na akaunti za muda maalumu anakuwa yuko salama zaidi, hasa katika hati fungani za serekali.

“Kwa hivyo tunaweza sema dhoruba zina kwenda sambamba na pale tunapowekeza, ni kazi yetu kuhakikisha tunakabiliana na mawimbi makali na ya wastani sababu lazima yawepo na kuhakikisha chombo kinafika salama. Utaalamu wa hali juu na uzoefu pamoja na sifa nyingine ndo tiba.

Mbaga anasema kwa kuwekeza katika sehemu tofauti tunapata faida kwa kuwa hizi sehemu tofauti zinakuwa na tabia tofauti pia.

Anato mfano kuwa mara nyingi hisa zinapokuwa zinapanda, riba kwenye hati fungani hushuka. Hisa zinapopanda, wawekezaji hukimbilia kuzinunua kwani hujua watapata faida, lakini zinapodorora, wawekezaji hukimbilia katika hati fungani.

Cha kufanya ni nini?

Mambo ya kufanya, mosi ni kuthimini malengo yako ya kiuchumi/kifedha na kwa muda upi unafikiri utayafikia

Pili, tathimini uthubutu wako katika Uwekezaji , utadhoofika kiasi gani kama faida au hata mtaji utapungua na tatu, tathimini gharama ziendanazo na Uwekezaji mzima

Jambo la kuepuka, ni kuchagua mfuko kwa kigezo tu kwamba unafanya vizuri kwa wakati huo. Yaweza kufanya hivyo kwa sababu tu ya faida muda mfupi.

Kitu kingine muhimu ni kufanya utafiti, kwanza pata historia ya mfuko na jaribu kuangali hali ya kibiashara ya sasa na baadae.

Aidha, jaribu kupata ushauri kabla ya kuwekeza, tafuta wajuzi wa Uwekezaji wa namana hii kabla ya kuthubutu. Kwa kifupi njoo tuongee.

Pia, kumbuka bei ya kipande inaendana na mwendo wa soko, kipande kina weza pand au kikashuka. Hivyo basi thamani ya kipande ina panda na kushuka.

Jambo muhimu la kuzingatia, ni kwamba kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS inasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMCA), kazi kubwa ya Mamlaka ikiwa kuhakikisha kuwa taratibu za msingi za Uwekezaji pamoja na mashart yake vinafuatwa ili kuepusha athari yeyeto ile kwa Mwekezaji.

Pamoja na Mamlaka, kuna wahasibu wa serekali, kampuni binafsi na wandani, pia kuna Mwangalizi CRDB Banki na Mkutano Mkuu wa Wawekezaji kila mwaka vyote hivyo, pamoja na utawala bora vikiwa ni kuona Mwekezaji anapata haki zake kutokana na hali halisi na kama ilivyo ainishwa katika Waraka wa Makubaliano.

Kwamba, baada ya kuangalia tahadahri za Uwekezaji wa pamoja itakuwa vyema kuangalia faida zake.

Kitaalamu, ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuwa na utaalamu wa juu ya Uwekezaji kwenye masoko ya hisa na mitaji, hivyo UTT AMIS kama mtaalamu anakusaidia hata kama ungependa kuwekeza wewe kama wewe.

Anuai, hata kama ni kiasi kidogo cha fedha kitawekezwa sehemeu mbali mbali hivyo basi kupunguza athari za Uwekezaji, mayayi yankuwa yameweka katika vikapu vingi.

Mtaji, sio lazima uwe na hela nyingi kama mtaji, kuanzia shilingi 10,000 tayari unakuwa ndani ya Uwekezaji. Pia, uwazi, unajua thamani ya mifuko na amana zako kila siku

Ukwasi, hakuna urasimu pale unahitajio sehemu au fedha zako zote; Kodi, unafuu wa kodi kwenye pato la mwisho; Gharama, gharama ndogo za uerndeshaji; Muda, unaendelea na shughuli zako zingine wakati meneja-UTT AMIS anasimamia Uwekezaji wako.

Mbaga anasema, baada ya kufahamu faida na hasara, anawasihi watanzania sasa waanze kuwa mwekezaji.


“Kwanza kabisa weka lengo-kwanini uwekeze, halafu tengeneza kanuni au taratibu itakayo kufikisha kwenye lengo lako.

“Chagua mfuko unaona una kufaa. UTT AMIS ina mifuko 5, yaani Umoja, Watoto, Wekeza Maisha, Jikimu, Ukwasi na pia ina huduma ya Usimamiziwa Mali (Wealth Management Service).

“Wekeza kwa muda mrefu unavyo weza ili kuipa faida jumusihi nafasi, na pia kuweza kununua vipande katika bei tofauti tofauti, ukisha nunua vipande usiache kuendelea kuongeza, nunua mara nyingi kadri unaweza.

Mbaga anamaliza kwa kukumbusha kuwa bei ya kipande inaweza panda au kushuka kutokana na mwendo wa soko.

No comments:

Post a Comment

Pages