Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dk. John Jingu
akifurahia jambo mara baada kuanza kazi Makao Makuu Mapya ya Wizara yake
yaliyoko eneo la Mtumba nje kidogo ya Jiji Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Bi. Mwajuma Magwiza wa Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii mara ya kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko
Mtumba nje Kidogo ya Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Bw. Leornard Mchau
mara ya baada kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko Mtumba nje
Kidogo ya Jiji la Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii imeanza rasmi kutoa huduma za Ofisi katika mji wa Serikali
uliopo Mtumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma na kuwataka wananchi kufuata
huduma za kiofisi katika ofisi hizo mpya. .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kimsingi Ofisi yake kwa sasa inatoa huduma zake katika ofisi zake zilizoko Mtumba na kuwataka wateja wake kufuata huduma hapo ambazo zitakuwa wazi muda wote
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kimsingi Ofisi yake kwa sasa inatoa huduma zake katika ofisi zake zilizoko Mtumba na kuwataka wateja wake kufuata huduma hapo ambazo zitakuwa wazi muda wote
.
"Nawakaribisha sana wananchi wote kuanza kutumia ofisi zetu hapa eneo la Mtumba na tuko hapa kama hatua muhimu ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais kwa vitendo." Aliongeza Dkt.Jingu. .
Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Wizara na Rasilimali Watu Bw. Leornad Mchau amesema ni uamuzi muhimu sana wa kuweka Ofisi za Serikali mahali pamoja ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa haraka na kwa gharama nafuu. .
Ameusifu uamuzi wa Serikali kuwa wa msingi sana akitofautisha na Dar es Salaam ambapo Wizara za Serikali zilitapakaa maeneo mbalimbali ya Jiji lakini kwa sasa hata kama ukitokea Jijini Dar es Salaam ni rahisi kupata huduma za Serikali katika eneo moja.
"Nawakaribisha sana wananchi wote kuanza kutumia ofisi zetu hapa eneo la Mtumba na tuko hapa kama hatua muhimu ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais kwa vitendo." Aliongeza Dkt.Jingu.
Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Wizara na Rasilimali Watu Bw. Leornad Mchau amesema ni uamuzi muhimu sana wa kuweka Ofisi za Serikali mahali pamoja ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa haraka na kwa gharama nafuu.
Ameusifu uamuzi wa Serikali kuwa wa msingi sana akitofautisha na Dar es Salaam ambapo Wizara za Serikali zilitapakaa maeneo mbalimbali ya Jiji lakini kwa sasa hata kama ukitokea Jijini Dar es Salaam ni rahisi kupata huduma za Serikali katika eneo moja.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Idara ya
Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza
ametoa rai kwa uongozi wa Jiji la Dodoma kuharakisha miundombinu ya usafiri ili
wananchi wanaoitaji huduma za kiofisi waweze kufika katika eneo la Mtumba na
kupata huduma hiyo kwa haraka.
Bi. Magwiza ameongeza kuwa kwa maoni
yake wateja watu wanahitaji miundombinu rafiki ili waweze kuhudumiwa na ofisi
yake kwa haraka lakini ana imani uongozi wa Jiji utaharakisha au kulifanyia
kazi jambo hili na kuwezesha wananchi kupata huduma ya haraka na kuwataka kuweka tayari mipango miji ili wawekezaji
waweze kuwekeza jilani na eneo hilo.
Wizara za Serikali tayari zimeanza kutolewa katika Jiji jipya la Serikali kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka Viongozi wa Setikali kuanza kutoa huduma zao Mtumba baada ya kukamilika kwa Ofisi hizo.
No comments:
Post a Comment