HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 01, 2019

YANGA KUIVAA NDANDA BILA AJIB

Nyota 20 wa kikosi cha mabingwa wa kihistoria  nchini, Yanga  SC, kitaanza safari ya kueleka Mtwara tayari kwa mchezo wa  ligi dhidi ya wenyeji Ndanda Fc, mchezo uliopangwa kutimua vumbi, April 4 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa nahodha  Ibrahim Ajib ataendelea kukosekana  kikosini kupisha majeraha madogo  aliyo nayo huku Juma abdul akirejea kikosini baada ya kupona majeraha
yake.


"Ibrahim Ajib bado tutaendelea kumkosa kikosini kutokana na majeraha ya  mguu, lakini jambo jema ni kwamba Juma Abdul amerejea kikosini na atakuwa  sehemu ya msafara wa kikosi chetu,mchezo utakuwa mgumu lakini maandalizi
tuliyoyafanya yanatosha kutupa matokeo mazuri".

No comments:

Post a Comment

Pages