Almasi
Yenye Thamani ya Bilioni 3.2 Yaipaisha Sekta ya Madini Tanzania.
Na
Mwandishi Wetu
Tanzania imetajwa kuweka historia katika
tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika
eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga na kuuzwa
kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.
Akizungumza katika mahojiano
maalum kuhusiana na madini hayo,Naibu
Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus
Nyongo amesema kuwa kutokana na
kupatikana kwa almasi hiyo Serikali itapata mapato ya takribani shilingi milioni 235,000/- kama kodi na tozo
mbalimbali ikiwemo mrabaha ambayo yamelipwa Serikalini baada ya mauzo hayo.
Kuuzwa kwa jiwe hilo moja la
almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni muendelezo wa tija
inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa kwake nchini,jumla ya
shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara ya dhahabu iliyofanyika
katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu
katika masoko ya madini kote nchini, kwa mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko, aliyetoa
taarifa hiyo hivi karibuni.
“Natoa wito kwa wachimbaji
wote,madalali na mawakala,kuyatumia ipasavyo masoko hayo kwakuwa kila mmoja
atapata stahiki yake tofauti na awali kabla ya kufunguliwa kwa masoko hayo
ambapo wachimbaji hawakuwa kwenye mikono salama kufutia kutokuwa na mfumo rasmi
wa uuzaji madini yao”.Alisisitiza mhe. Nyongo.
Akifafanua amesema kuwa kila
mchimbaji anapaswa kuzingatia sheria na Kanuni za sekta ya madini ili kuepuka
mkono wa sheria na hatua nyingine ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa madini yao
pale watakapobainika kutaka kutorosha madini ama kujihusisha na magendo.
Aliongeza kuwa baada ya kupatikana
kwa almasi hiyo wataalamu wa Wizara hiyo walifanya tathmini ili kuona ubora
wake na kiwango kilichopatikana ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato
yake.
“ Serikali ya Awamu ya Tano
imeweka makazo katika kuimarisha sekta ya madini nchini ili itoe mchango
unaostahili katika uchumi wetu ndio maana tunaona kuwa kupitia masoko ya madini
tuliyoanzisha hata mchimbaji huyu aliyepata hii almasi pale Maganzo aliiuza
kupitia soko letu la madini baada ya kufuata taratibu zote” alisisitiza Mhe.
Nyongo.
Tanzani ni moja ya nchi zenye
utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Almasi, Tanzanite, Dhahabu
na mengine mengi.
Serikali ya Awamu ya Tano imeweka
mkazo katika kuimarisha sekta ya madini ikiwemo kuimarisha taratibu za uuzaji
wa madini yote yanayozalishwa hapa nchini, kuimarisha usimamizi, kuwawezsha
wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba kwa tija.
No comments:
Post a Comment