HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2019

Waziri Biteko ashuhudia makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa Mwanza


Na GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameshuhudia makabidhiano ya mali ikiwemo dhahabu iliyokamatwa katika Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, ikisafirishwa kinyume na sheria baada ya kutaifishwa na mahakama kuwa mali ya Serikali.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 31, 2019 jijini Mwanza baina ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khatibu Kazungu.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko amewasihi wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuachana na utoroshaji wa madini kwani biashara hiyo kwa sasa ni zilipendwa hivyo wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.

Naye DPP Biswalo Mganga amesema mali zilizotaifishwa ni dhahamu kilo 319 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.018, fedha taslimu shilingi 305, mzani wa kupimia ubora wa madini, mizani ya kupimia madini pamoja na magari mawili ambapo vyote kwa pamoja vilikamatwa mwezi januari mwaka huu wilayani Sengerema. Aidha ameongeza kwamba dhahabu kilo tano iliyokamatwa mkoani Geita nayo imekabidhiwa serikalini baada ya kutaifishwa pia.

Baada ya kupokea mali hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu Kazungu ametoa shukrani kwa mamlaka zote zilizofanikisha kukamatwa, kutoa ushahidi na kutaifishwa na kwamba zitatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Madini, Khatibu Kazungu (wa kwanza kulia) wakishuhudia vipimo vya madini yaliyokamatwa wilayani Sengerema kabla ya kufanya makabidhiano.
Makabidhiano ya mali hizo yamefanyika leo jijini Mwanza na kushuhudiwa pia na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Madini yaliyokamatwa yakipimwa kabla ya makabidhiano kufanyika, hatua hii inajiri maada ya mahakama kutaifisha madini hayo.
Watuhumiwa 12 wakiwemo wenye mali wanne na askari polisi wanane walikamatwa wakihusishwa kuhusika na utoroshaji wa madini hayo wilayani Sengerema ambapo wenye mali walipatikana na hatia na kuhukumiwa huku askari polisi wakikana mashtaka dhidi yao ambapo bado kesi yao inaendelea mahakamani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakishuhudiano vipimo vya madini hayo kabla ya kufanyika makabidhiano.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia makabidhiano ya madini hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini.

No comments:

Post a Comment

Pages