Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya awali wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Kilimo ambao ni wajumbe wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU.
Na Mathias Canal, Wizara
ya Kilimo-Dodoma
Awamu
ya Tatu ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa (2017-2022 ina mtizamo mpya
unaolenga kuhakikisha kuwa rushwa inaondolewa nchini kwa kutumia mbinu mpya na
zinazotekelezeka kwa kuweka mkazo katika sekta zenye mazingira shawishi ya
rushwa.
Utekelezaji
wa Mkakati huo unalenga kupunguza na kudhibiti rushwa katika sekta/ maeneo
muhimu ya kimkakati ambayo ni pamoja na manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato,
utoaji wa haki, maliasili na utalii, madini, nishati, mafuta na gesi, afya,
elimu na ardhi.
Rushwa
ni adui wa haki, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya
Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019 amekemea na kuwataka watumishi
kupambana na rushwa katika sehemu za kazi.
Amewataka
watumishi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kutoshiriki katika kutoa
au kupokea rushwa. “Napenda kusisitiza kuwa yeyote atakayejihusisha na
kubainika kupokea au kutoa rushwa hatua stahiki na kali zitachukuliwa dhidi
yake” Alikaririwa Mhe Hasunga
Waziri
Hasunga amesema kuwa bado wizara
inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake kutoa
huduma kwa umma ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu wa
kutosha, hali inayosababisha kutofikiwa kwa malengo. “Niwahakikishie kuwa,
Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto hizo.
Ni matumaini yangu kuwa, mkiwa kama Wataalamu mtatumia uwezo wenu katika kuibua
mikakati itayosaidia kuwezesha Kilimo kuwa chenye tija na cha kibiashara” Alisisitiza
Kadhalika, amewataka watumishi wote kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa Umma.
Mhe Hasunga amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi
yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vinavyokiuka maadili
ya Utumishi wa Umma.
Serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inayo
dhamira ya dhati ya kuondoa uzembe na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma
na hivyo mtumishi anaruhusiwa kudai haki zile za msingi kwa kuzingatia Kanuni,
Sheria na Taratibu za Utumishi wa umma
wakati wa kutekeleza wajibu wake wa msingi kwa Mwajiri na kwa kutumia lugha ya
staha.
Vilevile
serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya Mwajiri na
watumishi kwani pasipokuwa na ushirikiano wa pande hizo mbili, ni vigumu
Taasisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Umuhimu huu wa mashirikiano, umetiliwa
mkazo kupitia Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia uendeshaji Taasisi za Umma.
Amesema
kuwa ili kuweza kutafsiri dhana hiyo,
ni muhimu pia kwa pande zote mbili kutambua haki na wajibu katika utekelezaji
wa majukumu ya kazi, kwani umekuwepo utamaduni wa baadhi ya watumishi kudai
haki bila kutimiza wajibu wao kwa Mwajiri.
No comments:
Post a Comment