Na
Farida Ramadhani na Peter Haule, Dodoma
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kiasi cha shilingi bilioni 6.8 ikiwa
ni gawio linalotokana na uwekezaji wa asilimia 21 za hisa katika Benki ya CRDB,
ikiwa ni sehemu ya shilingi bilioni 10 ambazo benki hiyo imetoa kama gawio kwa mashirika
na taasisi mbalimbali za umma zenye hisa katika Benki hiyo kutokana na faida
iliyopatikana Mwaka 2018.
Makabidhiano ya mfano wa
hundi za gawio hilo yalifanyika jijini Dodoma ambapo Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) alipokea gawio hilo kwa niaba ya
Serikali na kukabidhi baadhi ya mashirika na taasisi za umma zilizopata gawio
kutoka Benki hiyo.
Akizungumza katika hafla
hiyo Dkt. Mpango, aliupongeza uongozi wa benki hiyo kwa kurudisha fadhila kwa
mwananchi na kuzitaka benki na taasisi zote za fedha nchini kuiga mfano wa
benki hiyo kwa maendeleo ya nchi.
“Benki ya CRDB na benki
zingine muongeze jitihada ili kuongeza gawio kwa Serikali ili iweze kuwahudumia
wanachi katika huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu na maji”, alieleza Dkt. Mpango.
Alizitaka benki na taasisi
za fedha kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa huduma za benki ili waweze
kujikomboa kiuchumi na kuiwezesha nchi kupata gawio kwa ajili ya kugharamia
shughuli za maendeleo.
Dkt. Mpango aliipongeza
benki hiyo kwa kuwekeza katika teknolojia hasa katika matumizi ya Mfumo wa
Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroni (GePG) na kuzitaka benki na taasisi
zingine za fedha kutumia mfumo huo.
Aidha, Dkt. Mpango alipongeza
taasisi na mashirika ya umma yaliyopata gawio kutoka benki hiyo huku akizitaka
Serikali za Mitaa nchini kuiga mfano wa Halmashauri za Lindi, Shinyanga na
Mbinga ambazo zimepata gawio, ili ziweze kujiendesha na kukuza uchumi wa nchi.
“Serikali za Mitaa
zinaweza kufanya njia nyingine mbadala za kujiongezea kipato kama hii ya kuwekeza
kwenye Sekta ya fedha “, alisistiza.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Ally Laay alisema kuwa katika kipindi cha
mwaka 2018, Benki yake ilitengeneza faida ya shilingi bilioni 64.1 baada ya
kukatwa kodi ikilinganishwa na faida ya sh. bilioni 36.2 iliyopatikana Mwaka
2017, huku akichagiza mafanikio hayo na matumizi ya mfumo wa Serikali wa malipo
kwa njia ya kielektroniki (GePG).
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela Alisema CRDB imewekeza fedha kwenye
mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji katika Mto
Rufiji mkoani Pwani na kwamba benki yake iko tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa
miradi mingine ukiwemo ujenzi wa Reli ya
Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR).
Mashirika na taasisi za
umma zilizopokea gawio ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF
(Bil. 2.4), Mfuko wa Hifadhi ya Taifa-NSSF (Mil. 111.5), Mfuko wa Mafao kwa
Wafanyakazi wa Serikali-GEPF (Mil. 56,7) , Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar-ZSSF (Mil. 6.5)
Mashirika na taasisi
nyingine zilizopokea gawio hilo ambalo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 21 baada ya kodi kwa mwaka 2018 ni Mfuko
wa Maendeleo Lindi -(Mil. 111.5, Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga (Mil. !.3),
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (Mil. 13.3 na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya-NHIF (Mil.243.5)
Aidha, Chama cha ushirika
wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi kimepokea gawio la shilingi milioni 228.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (katikati) akiwa
ameshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi na Shilingi 6.7
bilioni ikiwa ni Gawio la Serikali kutoka Benki ya CRDB, Jumla ya Gawio
ni TZS 9.9 bilioni kwa Serikali Kuu, Halmashauri, Taasisi na Mashirika
ya umma ambayo ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSF, NSSF, GEPF na ZSSF) -
TZS 2.6 bilioni, TAMISEMI (Halmashauri za Mbinga, Lindi, Shinyanga) -
TZS 133.7 milioni, Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) - TZS 243.5
milioni Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Tabora - TZS 228
milioni. wengine pichani kutoka kushoto ni Balozi wa Denmark
nchini, Einar Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya
CRDB, Ally Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Khatibu Kazungu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay, akieleza kuhusu Benki yake kutoa mikopo katika mradi wa maendeleo wa umeme wa mto Rufiji na ujenzi wa Reli ya Kisasa yenye kiwango cha kimataifa-SGR, wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali, mashirika na taasisi zake la Sh. bilioni 10 , katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiipongeza Benki ya CRDB, kwa kuwa Benki ya mfano kwa kutoa gawio la jumla ya Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi za umma zilizowekeza hisa zao katika Benki hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay, akieleza kuhusu Benki yake kutoa mikopo katika mradi wa maendeleo wa umeme wa mto Rufiji na ujenzi wa Reli ya Kisasa yenye kiwango cha kimataifa-SGR, wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali, mashirika na taasisi zake la Sh. bilioni 10 , katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiipongeza Benki ya CRDB, kwa kuwa Benki ya mfano kwa kutoa gawio la jumla ya Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi za umma zilizowekeza hisa zao katika Benki hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tano kulia), akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa taasisi, mashirika ya umma na Mamlaka ya Serikali za
Mitaa waliopata gawio kutoka Benki ya CRDB, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), akipeana mkono
na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela, baada ya hafla ya
Benki hiyo kutoa gawio la Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi
mbalimbali za umma, katika ukumbi wa
Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono
na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay,
baada ya kupokea gawio kwa niaba ya Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali
za umma la Sh. bilioni 10, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini
Dodoma.
Baadhi
ya wadau waliohudhuria katika hafla ya Serikali
kupokea gawio la Sh. bilioni 10 kutoka Benki ya CRDB, wakimsikiliza kwa
makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo
pichani), alipokuwa akizitaka Benki na taasisi zingine za Fedha kutumia mfumo
wa malipo kwa njia ya kielektroniki- GePG, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati), Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu
(kulia), Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen (kushoto),
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Ally Laay (wa pili
kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela (wa pili
kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine baada ya Benki ya CRDB
kutoa gawio la Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali za
umma, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment