Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert
Jonkergouw akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa wanahisa wa
Benki ya NMB uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert
Jonkergouw, akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 15, 2019, jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa wanahisa wa
Benki ya NMB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,
Albert
Jonkergouw, akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 15, 2019,
jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa wanahisa wa
Benki ya NMB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,
Albert
Jonkergouw, akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 15, 2019,
jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa wanahisa wa
Benki ya NMB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB,
Albert
Jonkergouw, akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 15, 2019,
jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa wanahisa wa
Benki ya NMB.
Dar es Salaam, Tanzania
Wanahisa wa Benki ya
NMB wameidhinisha kiasi kilichopendekezwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka
(AGM), uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Ikiwa ni matokeo ya
utendaji bora na uimara wa nafasi ya mitaji, malipo ya jumla ya gawio la
Shilingi Bilioni 33 (sawa na Shilingi 66 kwa kila hisa), yanafanana na sera ya
benki ya kulipa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya faida la jumla baada ya makato
ya kodi (PAT) katika gawio. Hili ni ongezeko la asilimia 3 ukilinganisha na bei
ya Shilingi 64 kwa kila hisa iliyolipwa mwaka uliopita. Nia ni kukuza kiwango
cha gawio kwa kila hisa, kulingana na utendaji bora wa benki unavyoongezeka.
Benki iliripoti faida
ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 142 kabla ya makato ya kodi (PBT), kwa mwaaka
wa fedha ulioishia Desemba 31 2018; ambayo ni ongezeko la asilimia 3 kutoka
faida ya Shilingi Bilioni 138 iliyopatikana mwaka uliotangulia. Licha ya mafanikio
yaliyopatikana, Bodi na Uongozi wa Benki ya NMB umeridhishwa na aina ya
mafanikio na mapinduzi chanya katika kipindi cha mwaka.
Mapinduzi hayo ni
pamoja na uzinduzi wa NMB KLiK, mikopo ya mshahara - ambayo ni bidhaa ya
kwanza ya benki kutoa mkopo kwa njia ya simu. Kuanzishwa kwa Mawakala zaidi ya
6800, wanaoshughulika – pamoja na mambo mengine, ukusanyaji na ulipaji wa kodi,
ushuru na mapato ya Serikali za Mitaa katika Halmashauri 180, mapinduzi
yanayochangia mzunguko wa pesa kwa mifumo ya kidijitali na kukuza amana. Pia
tumeimarisha huduma za kibenki kupitia mtandao ilikuhudumia vizuri zaidi
akaunti za makampuni na kuwapa suluhisho
zote kamilifu na kufanya miamala ambayo imesababisha ongezeko la wateja kutoka
milioni 2.2 hadi milioni 3.1 mwishoni wa mwaka 2018 .
Uimara wa NMB kama taasisi
za fedha imepelekea Moody kuipa alama ya B1 ambayo vimethibitisha kuaminiwa kwa
Benki ya NMB na wawekezaji wa kimataaifa. Benki imeimarishwa vema na uwiano wa
mtaji kwa asilimia 16.5.Hiyo inamaanisha kwamba benki yetu iko salama kabisa
kibiashara Mwenyekiti wa Benki, Prof.
Joseph Semboja, anabainisha kuwa Bodi inataka kuweka sawa ongezeko la
wanahisa, sambamba na kuimarisha biashara ya fedha ndani ya benki katika mpango
mkakati wa kukua zaidi kiuchumi.
“Kwa miaka kadhaa sasa
NMB imeendelea kuwa imara yenye afya kifedha, lengo ni kuendelea kuimarika
zaidi na kubaki hivyo. Ili kufikia mafanikio haya, tunapaswa kuhakikisha
tunafanya maamuzi sahihi hasa katika udhibiti wa mabadiliko kwenye mahitaji
makuu ya kimtaji,” anasema Mwenyekiti.
“NMB imejipambanua
katika kuendelea kusaidia harakati za maendeleo ya uchumi Tanzania na kuvuka
kiwango cha sasa cha dira ya uchumi kama kichocheo cha ujenzi wa miundombinu ya
kiuchumi nchini. Tutaendelea kuwa vinara wa hudumaa bora kwa wateja wetu, huku
tukiendelea kutimiza wajibu wetu kwa jamii,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw.
NMB imejitolea katika
kusaidia ukuaji kiuchumi wa wajasiriamali wadogo na wakati (SME's), hususani
wanawake kwa kuwapa mafunzo na elimu ya uwezeshaji katika kuimarisha biashara
zao kwa kutambulisha jukwaa jipya la ‘Woman in Banking’ kote nchini. Katika
kilimo, NMB tumeboresha jopo la wataalamu wanaojikita zaidi katika Sekta ya
KilimoBiashara, ili kuimarisha mnyororo wa thamani unaopewa usaidizi mkubwa na
Taasisi ya NMB Foundation, ambayo inatoa elimu katika Taasisi za Sekta ya
Kilimo.
"Sisi ni Benki
Bora Tanzania. Ubora wetu ni katika nyanja zote, za utawala, teknolojia ya
habari na mfumo mzima unaoifanya NMB kuwa benki salama nchini, huku
tukihakikisha amana na akiba zako ziko salama chini yetu," aliongeza.
No comments:
Post a Comment