Mshambuliaji wa timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela akimtoka mlinzi wa
timu ya Soka ya Bunge, Rajab Kapira katika mechi ya kirafiki
iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma June 16, 2019. CRDB
ilishinda 3-1.
Waziri Mkuu Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa Timu
ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo, Abdulmajid Nsekela, kikombe cha ushindi wa mechi ya soka ya
kirafiki kati ya timu hiyo na timu ya Bunge iliyochezwa kwenye uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mchezaji nyota wa
timu ya mpira wa pete ya Bunge, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,
Mama Salma Kikwete kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki kati ya Bunge
na CRDB iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 16,
2019. Bunge ilishinda 35-2. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete akijiandaa
kurusha mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu ya Mpira wa Pete ya
Bunge na timu ya Benki ya CRDB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma,
Juni 16, 2019. Bunge ilishinda 35-2.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka ya benki ya CRDB wakishangilia
baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi baada ya kuitandika timu ya
Bunge 3-1 katika mechi ya kirafiki ilichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri
jijini Dodoma, Juni 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
No comments:
Post a Comment