Na Janeth Jovin
MTOTO
wa marehemu Mchungaji wa dhehebu la Evangelist Assemblies of God
(EAGT), John Mfuko, ajulikanaye kwa jina la Frida Mfuko, amefunguliwa
kesi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Temeke kwa kile
kilichoelezwa kuwa amevamia eneo lililoko keko juu katika kiwanja Na.
154 Plot II (Temeke) ikidaiwa kuwa kiwanja hicho ni mali ya dhehebu
hilo la EAGT.
Kesi hiyo
Na. 127 ya 2019 ipo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza Amina. Aidha, dhehebu
la EAGTE, imeonekana kuwa ni mdai namba moja katika kesi hiyo.
Wadai
wengine ni Mchungaji Sara Samson (ambaye pia amesema kuwa ni mdhamini
wa muda wa dhehebu la EAGT), Wilbroad Adebe na Enosi Ndembeta ambao ni
wazee wakanisa lililoko katika eneo hilo linalogombaniwa, wote kwa
ujumla wakidai kuwa mtoto wa marehemu Mzee Mfuko, amevamia eneo hilo.
Akizungumza
na blog hii, frida Mfuko anasema kuwa baba yake ni mmoja wa waazilishi
wa dhehebu la EAGT tangu 1993 baada ya kutokea kwa mgogoro mkubwa katika
kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).
Anasema
marehemu Mchungaji Mfuko amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa
EAGT hadi pale kifo kilipomkuta tarehe Agosti Mosi mwaka jana.
Kwa
mujibu wa msemaji huyo wa familia amedai kuwa tarehe Mei 9, 2013
wajumbe watatu wa bodi ya wadhamini walikaa kikao na kuidhinisha pamoja
na mambo mengine kuwa, kiwanja na. 154 kilichopo katika Kitalu II, Keko
Juu, Manispaa ya Temeke si mali ya EAGT bali ni mali ya Marehemu
mchungaji Mfuko na hivyo wadhamini waliaamua kumilikisha kiwanja hicho.
"Baraza
la wadhamini lilifanikiwa kuandaa nyaraka za kubadilisha hati ya
kiwanja hicho na kumilikisha rasmi marehemu mchungaji John Henry Mfuko
na hivyo hati ya kiwanja ikabadilishwa kutoka jina la The Registered
Board of Trustees of EAGT, na kuwekwa jina la John Henry Mfuko kama
miliki halali wa kiwanja hicho na shule iliyopo katika kiwanja hicho
amabayo pia imesajiliwa kwa jina hilo la mchungaji," anasema
Aidha,
watoto wa marehemu mchungaji Mfuko wamelaani kitendo hicho cha
kuwataka kuwafukuza na kuwanyanganya mali ya baba yao ikiwa viongozi wa
EAGT wanajua fika kuwa kiwanja kile pamoja na majengo yaliyopo na shule
ni mali ya marehemu baba yao .
Aidha,
msemaji wafamilia ameiambia blog hii kuwa, viongozi wa EAGT, wanafanya
unyama huo kwa sababu marehemu mzee mfuko kabla ya kufariki dunia
alikuwa akihoji viongozi wakuu wa kanisa la EAGT kuhusu tuhuma za
kuingiza magari nchini kwa kutumia jina la EAGT ikiwa magari hayo hayapo
ndani ya umiliki wa dhehebu hilo ikiwa kuna ukwepaji wa kodi ya
serikali.
Baadhi ya
washirika na wachungaji wa dhehebu la EAGT waliohojiwa walisitikishwa
na kidendo hicho huku wakisema kuwa marehemu Mzee mfuko alikuwa nguzo
muhimu katika dhehebu la EAGT na hivyo kuwanyanyasa watoto wake ni
kutafuta laana.
Aidha
wamesikitishwa na vurugu zinazoendelea ndani ya dhehebu la EAGT kwa muda
mrefu sana ambapo wachungaji wanafukuzwa katika makanisa yao na
serikali haijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo.
Wakati
yote hayo yakiendelea viongozi wa EAGT wamekumbwa na tuhuma nzito
zikiwemo za kuingia mikataba isiyowazi ya kupangisha majengo ya Makao
Makuu yaliyopo Dar es Salaam Katika kiwanja namba 1 Barabara ya nyerere.
Kwa
mujibu wa mpangaji katika eneo hilo (Imalaseko Super Market ) kupitia
barua yake ya tarehe 3/4/2018 (kumb. Na. IIL/GN/003/2018) ni kuwa;
kampuni hyo ilipewa jukumu la kujenga majengo hayo na kisha kuyatumia
hadi hapo itakapokuwa imejirejeshea gharama za ujenzi .
Hivyo
kufikia tarehe 1/8/2018 Kampuni ya Imalaseko Investment Limited
ilikuwa imekaa katika majengo hayo kwa kipindi cha miaka saba (7) na
ilikuwa imeweza kujireshea kiasi cha sh. 422, 204,720/= na hivyo kuwa
bado indai kiasi cha sh. 2,416,204,720/.
Kwa
mujibu wa Mchungaji John Mahene, ambaye ni Makamu Askofu Mkuu wa EAGT,
anasema kuwa si kweli majengo ya EAGT yalijengwa tu kwa gharama za
Imalaseko Investment Limited bali makanisa yote nchini yalichangishwa
ilikufankisha ununuzi wa kiwanja na majengo hayo.
No comments:
Post a Comment