Mtaalamu wa Afya
akimhudumia mmoja wa wasafiri waliokuwa
wakipita katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga aliyeigiza
kuugua, wakati
wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
Na OWM, NAMANGA
Kufuatia zoezi
linaloendelea mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linajikita
katika Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019, Wataalamu
wa sekta za Afya wa Tanzania na Kenya, katika makundi tofauti wameweza
kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika Kupima kwa vitendo
hatua za kujiandaa na kukabili Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa.
Wataalam hao
wameweza kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya
Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya
Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza
madhara ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa kwa Wanyama na Binadamu.
Zoezi hilo,
linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya
binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na
kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu.
No comments:
Post a Comment