HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2019

RAIS WA DRC FELIX TSHISEKEDI AWASILI TANZANIA

 Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi akikabidhiwa Ua la ishara ya Upendo na kumkaribisha Nchini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Pombe Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
 Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi akikagua paredi maalumu aliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Pombe Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
Gwaride maalumu lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Pombe Magufuli wakitoa heshima katika hafla ya mapokezi iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wakitazama kikundi cha ngoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakiwapungia mikono wananchi waliojitokeza katika sherehe za kumkaribisha Rais wa Kongo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akizungumza  na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli akipokea zawadi kutoka kwa  Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt. Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli akimkabidhiu zawadi ya Picha ya Wanyama Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt.Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akiwa  Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John  Pombe Magufuli akimtambulisha Rais wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi kwa Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam katika Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt.Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam. Junin 13, 2019. Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Pages