HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 29, 2019

DPP AKABIDHI MADINI, VITO NA FEDHA BOT ZILIZOTOKANA NA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika vipindi tofauti kati ya mwaka 2017 na 2018 imeendesha kesi mbalimbali zinazohusiana na Utotoshaji au kukutwa na madini bila kuwa na kibali.
Katika uendeshaji wa kesi hizo,Washitakiwa walitiwa hatiani na kuamriwa kulipa faini aua kutumikia kifungo gerezani pamoja na amri ya kutaifisha madini na fedha walizokamatwa nazo wakati wakisafirisha madini hayo. 

Madini yaliyotaifishwa ni Kilo 25.546 za dhahabu, zaidi ya kilo 76.020.20(Tani 76) za Colored gemstones, Tanzanite pamoja na fedha za kigeni za mataifa mbalimbali kumi na tano (15) zenye thamani ya TZS 1,023,608.515.12
Kwa kuwa madini hayo yametunzwa sehemu mbalimbali kiasi kwamba uwezekano wa kupotea au kumbukumbu zake kupotea, na kwa kuwa mali zote zinazotaifishwa zinakuwa ni mali za serikali ambapo katibu mkuu Hazina ndiye msimamizi wa mali hizo. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amekabidhi Kilo 25.5 za Dhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani 915,954.72 sawa na Sh. Bilioni 2,102,095,941

Madini/Vito
1.    Tani 76 na Carrats 2849 zenye thamani ya Dola 2,638,349.95 sawa na Sh. Bilioni 6,068,204.885
2.    Carrats 2,849 zenye tahamani ya Dola 3,803.32 sawa na Sh.Bilioni 888,409.000
3.    Tanzanite gramu 888 zenya thamani ya Dola 3,197 sawa na Sh.Bilioni 7,353,348(hazijakabidhiwa leo)
4.    Fedha za kigeni za Mataifa 15 mbalimbali ambazo ni sawa na Sh.Bilioni 1,023,608,515.12

Jumla kuu thamani ya madini na Fedha ni Sh.3,125,704,456.12
Masanduku yaliyoifadhiwa Madini,Vito pamoja na fedha za Mataifa mbalimbali zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi zikiingizwa Ukumbini tayari kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga kukabidhi kwa Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali  sehemu ya vipande vya Madini ya Dhahabu ambayo ilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Agustine Mahiga, Waziri wa Madini Dotto Biteko pamoja na Kamishina wa Madini Profesa Abdukalim Mruma wakiwa wamishika vipande vya madini ya dhahabu ambayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amezikabidhi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, vito na Fedha za mataifa mbalimbali zilizokamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akionyesha juu kwa Mawaziri na Wanahabari Fedha za Kimarekani (Dollar) kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Fedha hizo pamoja  na Madini na Vito ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali  sehemu ya Fedha za Mataifa mbalimbali pamoja  na Madini na Vito ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akionyesha juu kwa Mawaziri na Wanahabari moja kipande cha madini ya Pie light kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, Vito na Fedha za mataifa mbalimbali  ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akikagua sehemu ya fedha za mataifa mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa kwa  niaba ya Serikali Fedha na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amabazo zilikamatwa  na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini vikiwemo pia Madini na vito mbalimbali, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
Picha namba 14. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa kwa  niaba ya Serikali Madini, vito mbalimbali na Fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa  na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Agustine Mahiga akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi Madini, vito mbalimbali na Fedha kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa  na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi Madini, vito mbalimbali na Fedha kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa  na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Pages