Meneja wa Bar ya Shine Pub ya mkoani Iringa, Richard Sanga, akitoa kero yake mbele ya wanahabari. (Picha na Denis Mlowe).
Mmoja wa wamiliki wa bar akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya walipofika ofisini kwake kuzungumza juu ya malalamiko ya jeshi la polisi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza na wamiliki wa bar na mameneja mara baada ya kuwasikiliza malalamiko yao ya kufanyiwa vurugu na polisi nyakati za usiku.
Na Denis Mlowe, Iringa
WAMILIKI wa bar na klabu za usiku mkoani Iringa wamepinga na kulalamikia kitendo cha jeshi la polisi mkoani
Iringa kuwafanyia vitendo vya kupiga wateja na wahudumu kwa kile
kinachosemekana muda wa kufunga bar kuzidishwa.
Wakizungumza mara
baada ya kuandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela,
wafanyabiashara hao Zaidi ya 30 wanaomiliki bar mkoani hapa walisema kuwa
kitendo kinachofanywa na baadhi ya askari wa jeshi hilo wanaofanya doria
nyakati za usiku wamekuwa wakiwapiga wateja na wahudumu pindi wakikuta muda wa
kufunga bado ni kitendo kinachohatarisha Amani.
Mmoja wa
wamiliki wa Bar mkoani hapa
aliyezungumzia hali hiyo, Happy Matanji alisema kuwa tarehe 8 mwezi huu
walipita polisi katika bar anayomiliki wakaamuru bar ifungwe lakini walitumia
nguvu kubwa na kuanza kuwapiga wateja na
wahudumu na kila mtu aliyeonekana katika eneo hilo licha ya kuwa na kibali
kinachoruhusu kutoa huduma muda wa zaida.
Alisema kuwa
manispaa walimpatia kibari ambacho nikaruhusu kufunga bar hiyo hadi saa nane
badala ya muda wa saa sita lakini askari waliokuwa doria hawakutaka kabisa
kusikiliza wala kukubaliana na kibari
ambacho kinaruhusu kufungwa kwa huduma za bar kutokana na kibari hicho.
Alisema kuwa
meneja wa bar hiyo alichukua jukumu la kwenda kituo cha polisi kupata msaada Zaidi
lakini alipofika kituoni walimweka ndani kwa kumwambia kwamba hadi kituoni
amewafata licha ya kuwa kibali cha kufanya biashara hadi muda huo.
“Unaamua
kuepusha shari na kufata sharia ya kuomba kibali lakini cha kushangaza mamlaka
ya jeshi la polisi wanakuwa hawakitambui na mwisho wa siku wateja na wahudumu
wanaambulia kipigo hapo unakuwa unaingia hasara kubwa ya kulipia kibali na hela
kupotea na haitoshi wanapelekwa mahabusu sasa hapo inakuwaje” alisema
Alisema kuwa
alichukua jukumu la kumpigia kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa na
kumwabarisha kuhusu hali hali na kusema kuwa analifanyia kazi na kumjulisha
laki alipotafutwa siku ya pili hakuweza kupokea simu na juzi alipopigiwa rpc
alisema kuwa yuko katika kikao atapigiwa lakini hakuna hatua yoyote ile.
Matanji aliongeza
kuwa anashangaa kwa kiasi kikubwa ni mafunzo ya aina gani wanayopatiwa jeshi la
polisi kutumia nguvu kubwa katika kuwakabili wateja ambao hawana shida yoyote
hali ambayo inawashangaza wengi kwani hapo awali hali hii haikuwepo.
Richard Sanga
meneja wa bar ya Shine Pub alisema kuwa vitendo ambavyo wanafanya jeshi la
polisi limefanyika katika bar hiyo na kusema kwamba leseni za biashara
hazionyeshi ni muda gani wa biashara hiyo inafungwa saa ngapi tofauti na leseni
za zamani zilizokuwa zinaonyesha muda wa kufungua na kufunga hivyo unaambiwa tu
unatakiwa kufunga muda Fulani.
Alisema kuwa
polisi anapofanya kazi yake inabidi afate uongozi wa eneo husika na kufanya
mazungumzo kwamba muda wa kufunga umewadia ikiwezekana kumshauri na kumpa onyo
ila wao wakifika hakuna onyo wala ushauri wowote kikubwa ni nguvu mwanzo mwisho
na kutoa amri za watu kukaa chini licha yaw engine kuwa wamekaa hapo ndipo
hasara inaanza kwani wengi wa wateja wanakuwa wanadaiwa bili lakini nguvu
inayotumika ni kubwa.
Alisema kuwa
askari wanatembea na viboko, nyaya za umeme za kumpigia mtu bila kufikiria
kwamba raia ni askari jamii na wanafanya kazi kwa Amani iweje wao watumie nguvu
badala ya kujenga ushirikiano ambao utasaidia kuwabaini wahalifu na kuuweka mji
kuwa sawa lakini askari wa doria wakija wao na mabavu kwa kila mtu ndani ya bar
na kisha wanakamatwa na kupelekwa mahabusu.
Alisema kuwa
faini inayotolewa mahakamani ni kubwa Zaidi kuliko ilivyowekwa kisheria ambapo
unakuta mtu unalipa Zaidi ya laki sita kwa kuwalipia faini wahudumu sita wa bar
waliofikishwa mahakamani hapo na mbaya Zaidi wanakuwa hawana makosa kwa kuwa
wanakuwa wanakamatwa katika eneo la kazi lakini wanafunguliwa makosa uzembe na
uzururaji.
Sanga aliongeza
kuwa biashara wanayofanya wanakumbuna na changamoto nyingi sana ambazo nyingine
wanashindwa kukabiliana nazo zikiwemo utitiri wa kodi lakini licha ya hivyo
muda wa kufanya biashara mchache na hapo unakutana na changamoto nyingine ya
doria na wateja kuondoka na bili.
Akiwajibu wamiliki
wa bar waliofika ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela
alisema kuwa mzunguko wa fedha kwa asilimia kubwa unaletwa na wamiliki wa
sehemu za vinywaji na kukiri kuwa jeshi la polisi limefanya kosa na kuwaomba
msamaha kwa wamiliki wa bar na klabu kwa niaba ya jeshi la polisi.
Kasesela ambaye
na Mwenyekiti wa Usalama wa Wilaya ya Iringa alisema kuwa awali hakukuwa na
tabia kama hiyo hivyo ataongea na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa na
kubaini nini hasa chanzo ambacho kinasababisha haya yote ambayo yanatokea sasa
kwa wahudumu na wateja wa bar.
Alisema kuwa
kwa upande wa jeshi la polisi na serikali walitalifanyia kazi na kuwahakikishia
kuwa hakuna askari atakayepona endapo atabainika kuwanyanyasa Watanzania
wenzake bila sababu na kutangaza kwa wamilki wa bar na pub zote wilaya ya
Iringa mwisho wa kufunga ni saa sita na ikifika saa tano wamiliki wa bar wanatakiwa
kupunguza sauti ya muziki na ikifika muda was aa saba askari wasiwabugudhi
wateja.
No comments:
Post a Comment