Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, Paul Makonda, akizindua jezi itakayotumiwa na Taifa Stars katika AFCON 2019.
Taifa Stars iliyoichapa Uganda na kufuzu AFCON 2019.
Alexandria, Misri
KATIKA
kujiandaa na Fainali za Mataifa Afrika (AFCON 2019), kikosi cha timu ya Taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ leo saa 4:00 usiku (kwa saaa za Afrika Mashariki), kinashuka
dimbani mjini Alexandria, nchini Misri kuumana na wenyeji wao, kwenye Uwanja wa
Bourg Al Arab.
Taifa
Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inayozalishwa na Kampuni ya Serengeti
Breweries (SBL), ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Mnigeria Emmanuel Amunike, inajiandaa
kucheza fainali za pili za AFCON katika historia ya soka la Tanzania, baada ya
kufanya hivyo mwaka 1980.
Katika
fainali za AFCON 2019, Tanzania imepangwa Kundi C, pamoja na mataifa Algeria, Senegal
na Kenya. Kikosi
hicho ambacho leo kinazindua jezi mpya, kitaanza mechi zake tatu za Kundi C,
dhidi ya Senegal Juni 23, kisha kuivaa Kenya Juni 27 na kumaliza na Algeria
Julai 1.
Kikosi
cha wachezaji 23 wanaoendelea na mazoezi kujiandaa na fainali hizo ni Aishi Manula,
Metacha Mnata, Aron Kalambo, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Ally Sonso, Vicent
Phillipo, Mohammed Hussein ‘Tshabalala,’ Agrey Moris, Kelvin Yondani, Erasto
Nyoni na Feisal Salum ‘Fei Toto.’
Nyota
wengine wa Taifa Stars ni pamoja na Mudathir Yahaya, Yahya Zayd, Frank Domayo,
Saimon Msuva, Rashid Mandawa, Mbwana Samatta (nahodha), Thomas Ulimwengu, John
Bocco, Farid Mussa, Adi Yusuph na Himid Mao ‘Ninja.’
Fainali
za AFCON 2019 zitaanza kuunguruma Ijumaa ya Juni 21, ambako wenyeji Misri
wataumana na Zimbabwe, katika pambano la kundi A la michuano hiyo, ambayo kwa
mara ya kwanza inashirikisha mataifa 24 badala ya 16 yaliyokuwa yakishiriki
katika fainali zilizotangulia.
MAKUNDI AFCON 2019
Kundi A: Misri, Zimbabwe,
Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kundi B: Burundi,
Madagascar, Guinea na Nigeria
Kundi C: Tanzania,
Kenya, Senegal na Algeria
Kundi D: Namibia, Afrika
Kusini, Ivory Coast na Morocco
Kundi E: Angola,
Mauritania, Mali na Tunisia
Kundi F: Guinea Bessau,
Benin, Ghana na mabingwa watetezi, Cameroon.
No comments:
Post a Comment