HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2019

MANISPAA YA TABORA YATOA MKOPO WA MILIONI 80.5 KWA KIKUNDI

 Mkuu wa Wilaya Tabora Mhe. Erick Kitwala Komanya akisisitiza jambo jana wakati wa hafla fupi ya utoaji wa mikopo ya shilingi milioni 80.5 kwa vikundi 14 vikiwemo vya wanawake, vijana na walemavu kutoka Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Wilaya Tabora Mhe. Erick Kitwala Komanya (katikati), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Leopold Chundu Ulaya (mwenye shati ya kijani), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Joseph Kashushura (mwenye koti jeusi) wakiwa wameshika mfano wa hundi jana wakati wa hafla fupi ya utoaji wa mikopo ya shilingi milioni 80.5 kwa vikundi 14 vikiwemo vya wanawake, vijana na walemavu kutoka Manispaa ya Tabora.

 
NA TIGANYA VINCENT

JUMLA ya shilingi milioni 80.5 zimetolewa kwa ajili ya uwezeshaji wa vikundi 14 vya wanawake, vijana na walemavu katika Manispaa ya Tabora.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Sheria inayozitaka kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi hivyo.

Akikabidhi hundi za mkopo jana kwa vikundi, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Erick Kitwala Komanya alisema fedha walizokopeshwa zinapaswa kutumika kama chachu ya kuwaletea maendeleo.

Alisema ni vema fedha walizokopeshwa wanapaswa kuzitumia katika malengo waliyoombea na siyo kupeleka katika matumizi mengine kama vile starehe na anasa ambazo zitawafanya washindwe kurejesha.

Mhe. Komanya aliongeza kuwa wanatakiwa kurejesha fedha hizo kwa wakati ili vikundi vingine vya vijana , wanawake na walemavu waweze kukopeshwa kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na jamii inayowazunguka.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Leopold Chundu Ulaya alisema kuwa mikopo waliyopaya haina riba kwa hiyo wanapaswa kurejesha fedha kulinga na kiwango walichopata. 

Naye Naibu Meya Yahaya Mhamali alisema lengo na mikopo inayotolewa ni kuwakomboa vijana, wanawake na walemavu kutoka umaskini na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Nchi.
Alisema kuwa kikundi kitakachoresha mkopo kwa wakati kinapewa mkopo mwingine zaidi ya ule walioupata. Hadi kufikia sasa Manispaa ya Tabora imeshatoa milioni 226 kwenye mwaka huu wa fedha.

No comments:

Post a Comment

Pages