HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2019

RC TABORA AMSIMAMISHA MENEJA WA TRA IGUNGA KUPISHA UCHUNGUZI WA TUHUMA DHIDI YAKE

Na Tiganya Vincent

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imemusimasha Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani Igunga John Mgeni ili kupitisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa semina ya uelimishaji wa wafanyabiashara wilayani Igunga juu ya ulipaji kodi.

Mkuu huyo wa Mkoa alichukua hatua hiyo baada ya Mfanyabiashara mmoja kulalamikia kuwa alikutwa na kosa la kutotoa stakabadhi ya mauzo ya shilingi elfu 10 na kutakiwa kulipa adhabu (faini) ya shilingi milioni 4.5 au kupelekwa Mahakamani.

Aliongeza Meneja huyo alimwambia Mfanyabiashara huyo anaweza kumpa milioni mbili ili asipelekwe Mahakamani wala asilipe adhabu inayohitajika Kisheria.

Kufuatia tuhuma hizo Mkuu wa Mkoa aliagiza Mkuu wa Taasisi za Kuzuia na Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi na Meneja huyo kutoingia Ofisi ili kuwezesha kuwepo na uchunguzi huru.

Aidha Mwanri alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Igunga kuhakikisha ulinzi kwa Mfanyabiashara alifichua uovu ili asije akabughuziwa na kutishiwa maisha.

Kwa upande Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora Thomas Masese aliwataka wafanyabiashara kuwa huru kuwafichua watendaji wote wa Mamlaka hiyo ambao wanaendesha vitendo viovu na kusababisha ukusanyaji mbovu wa mapato ya Serikali.

Alisema TRA haitambughuzi mfanyabiashara yoyote ambaye amefichua uovu wa watumishi wa TRA.

No comments:

Post a Comment

Pages