HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2019

TRA TABORA YAKUSANYA BILIONI 19.989

Na Tiganya Vincent

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoani Tabora imekusanya jumla ya shilingi bilioni 19.989 katika msimu wa mwaka 2018/19 kutokana na mapato ya ndani.
Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 89 ya lengo la kukusanya bilioni 22.440 ambalo Mkoa wa Tabora ulikuwa umepangiwa. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora Thomas Masese wakati wa semina ya uelimishaji wa wafanyabiashara wilayani Igunga. 

Alisema kwa upande wa kodi za forodha umevuka lengo kwa kukusanya shilingi bilioni 38 .5 ambayo ni asilimia 838 ya bilioni 4.6. 

Masese alisema kwa upande wa kodi za forodha wamefanikiwa kuvuka lengo baada ya kukamata gari lililoingia Nchini kutoka nchi jirani bila kulipa ushuru wa forodha na kulipiga faini. 

Naye Meneja wa TRA wilayani Igunga John Mgeni alisema walifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.664 ambazo ni sawa na asilimia 94 ya lengo la bilioni 1.763 ya makusanyo. 

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka wafanyabiashara Mkoani humo kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiara ili Serikali iendelee kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages