MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikoa cha
baraza la
madiwani maalum la kujibu hoja za mkaguzi wa serikali CAG la Jiji hilo
kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akifuatiwa na Naibu Meya wa Jiji hilo Mohamed Haniu.
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Alhaji Mustapha Selebosi
DIWANI wa Kata ya Msambweni Jijini Tanga (CUF) Abdurahamani Mussa akichangia wakati wa kikao hicho

Sehemu ya Madiwani wa Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho. Tanga, Tanzania |
Serikali imepeleka kiasi cha sh Bil 8 kwa Halimashauri
ya Jiji la Tanga kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye
sekta za Afya na elimu.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, wakati wa baraza la
madiwani maalum la kujibu hoja za mkaguzi wa serikali CAG la Jiji hilo
lilofanyika hapo jana.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha wanatekeleza
miradi ya Maendeleo kwa wakati ili kumaliza kero zinazowakabili
wananchi.
"Mnachotakiwa
Halimashauri ni kuhakikisha fedha hizo zinatumika katika malengo
yaliyokusudiwa lakini na miradi hiyo iweze kuzingatia thamani halisi ya
fedha hizo"alisema RC Shigela.
Awali
akisoma hoja za CAG Mwekahazina wa Jiji la Tanga Corner Sima alisema
kuwa ucheleweshaji wa fedha kwa ajili yautekelezaji wa miradi ya
kimkakati yamajiji nchini umesababisha kushindwa kutekelezeka.
"Ucheleweshaji
wa fedha hizo ilisababishia kuibua hoja kutoka kwa CAG kwani katika sh
Bil 232.5 zilizotumwa kwa ajili yamiradi tuliweza kutumia sh Bil 4.7
sawa naasilimia 2% ya fedha hizo"alisema Sima.
Hivyo
ofisi ya CAG imeielekeza Halimashauri ya Jiji hilo kuwasilisha mpango
kazi wa matumizi ya fedha hizo na namna ambavyo zitaweza kutumika katika
kutekeleza miradi hiyo ya kimaendeleo.
Nae
Mstahiki Meya wa Jiji hilo Seleboss Mustafa alisema kuwa katika mwaka
huu wa fedha wamejipanga kusimamia kwa ukaribu mapato pamoja na kuibua
vyanzo vipya.
Huku
akitilia mkazo namna walivyojipanga kuhakikisha wanatoa mikopo yenye
masharti nafuu kwa makundi maalum ya vija a ,wanawake na Walemavu
walioko katika kata 21 za Jiji hilo.
"Tumekuja
na hari ya kuhakikisha tunamaliza changamoto za kimaendeleo kwa
wananchi wetu huku kipaumbele kikubwa ikiwa ni ukusanyaji wa mapato ili
kutekeleza miradi yetu ya Maendeleo na kuwaondolea adha wananchi
wetu"alisema Meya huyo.
No comments:
Post a Comment