HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2019

WANAWAKE IRINGA WATAKIWA KUTOWANYANYASA WANAUME WAKIPATA MAFANIKIO YA KIFEDHA

 Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Iringa, Happynes Seneda (katikati waliosimama mstari wa mbele),akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam waliokuwa katika ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao wa mkoa huo kujiunga na Umoja wa Kitaifa mjini humo mwishoni mwa wiki. Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa Ufadhili wa Ubalozi wa Uingereza.
Ofisa Biashara Biashara wa Manispaa ya Iringa , Benjamin Nyigu (katikati waliosimama mstari wa mbele),akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam waliokuwa katika ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao wa mkoa huo kujiunga na Umoja wa Kitaifa mjini humo mwishoni mwa wiki.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa Ufadhili wa Ubalozi wa Uingereza.
 Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam wakiingia Ofisi ya Meya Manispaa ya Iringa.
 Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa EfG, Penina Reveta akimkabidhi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe taarifa fupi ya shughuli zilizofanywa na shirika hilo
 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (katikati waliosimama mstari wa nyuma),akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam waliokuwa katika ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao wa mkoa huo kujiunga na Umoja wa Kitaifa mjini humo mwishoni mwa wiki.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa Ufadhili wa Ubalozi wa Uingereza.
 Wanawake Wafanyabiashara Masokoni wa jijini Dar es Salaam wakitembela Soko la Mashine Tatu katika Manispaa ya Iringa.
 Mwezeshaji Sheria Jane Nyanda kutoka Soko la Buguruni akizungumza na wanawake wa Soko la Mashine Tatu.
 Mwenyekiti wa Soko la Mashine Tatu, Jafari Sewando , akizungumza na wanawake wa Soko hilo wakati wa mkutano wa kuwahamasisha kujiunga na Umoja wa Kitaifa.  
 Picha ya pamoja na  Wanawake wa Soko la Mashine Tatu
 Mwanasheria wa EfG akizungumza na wanawake wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa 
 Ofisa Tathmini na Uwajibikaji wa EfG,  Samora Julius (kulia), akizungumza na wanawake wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa  mwishoni mwa wiki wakati katika mkutano wa uhamasishaji wanawake wafanyabiashara wa soko hilo kujiunga na Umoja wa Kitaifa.
 Mwenyekiti wa muda wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara Masokoni Kitaifa, Betty Mtewele, akizungumza n wanawake wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa wakati akiwahamasisha kujiunga na umoja wa kitaifa.
 Katibu wa Soko Kuu la Mkoa wa Iringa, Hamis Msimbe akizungumza
 Picha ya pamoja Soko Kuu la Mkoa wa Iringa.
 Ofisa Utawala wa EfG,  Eva Buhembo, akizungumza na wanawake wa Soko la Kihesa. 
 Mwenyekiti wa Soko la Kihesa katika Manispaa ya Iringa, Subira Mohammed, akizungumza.
Picha ya pamoja Soko  la Kihesa.


Na Dotto Mwaibale, Iringa

WANAWAKE Mkoani Iringa wametakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanaume mara baada ya kupata mafanikio ya kifedha.

Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki  kwa nyakati tofauti na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakati wakizungumza na timu ya wafanyabiashara wanawake kutoka Dar es Slaam ambao walikuwa kwenye ziara ya mafunzo na kufanya mchakato wa wafanyabiashara wanawake masokoni kuunda Umoja wa Kitaifa kupitia Shirika la Equality for Growth (EfG)

Akizungumza na wanawake hao Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa wa Iringa, Happynes Seneda aliwaomba wanawake hao kutosahau wajibu wao kwa waume zao baada ya kupata mafanikio ya kifedha.

" Mkifanikiwa kutokana na biashara zetu msiache majukumu yenu kwa waume zenu mimi mwenyewe hapa mnapo niona nina mtoto mchanga licha ya kuwa na majukumu mengi ya kiofisi nikifika nyumbani lazima nifanye majukumu yote ya familia yangu" alisema Seneda.

Seneda alitoa shukurani kwa EfG kwa kufika katika mkoa huo kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wafanyabiashara masokoni ili wawe na nguvu ya maendeleo katika kujiinua kiuchumi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe kwa nyakati nyingine naye alisisitiza wanawake wa mkoa huo kuacha tabia hiyo ya kuwanyanyasa wanaume pale wanapokuwa wamepata mafanikio na akatumia nafasi hiyo kulikaribisha shirika hilo kufanya kazi zake katika manispaa ya Iringa.

Katika hatua nyingine Mtunza Hazina wa Soko la Kihesa Venance Msigwa naye alirudia kuwaomba wanawake mkoani humo kuacha tabia ya kuwadharau na kuwanyanyasa wanaume pale wanapokuwa wamepata mafanikio.

Ofisa Tathmini na Uwajibikaji wa EfG,  Samora Julius alisema wamefanya ziara katika masoko tisa  ya jiji la Mbeya ambayo ni Soweto, Uyole, Nzovwe, Ilomba, Mabatini, Igawilo, Iyunga, Soko Matola na Uhindini kwa lengo la kuwahamasisha wafanyabiashar wanawake katika masoko kuunda umoja wa kitaifa utakao wasaidia kwa mambo mbalimbali na kuelezea mafanikio ya Mradi wa Sauti ya Mwanamke Sokoni ambao umefadhiliwa na Ubalozi wa Uingereza.

Alisema katika mkoa wa Iringa wametembelea masoko matatu yaliyopo ndani ya manispaa ambayo ni Mashine Tatu, Soko Kuu na Soko la Kihesa ambapo kwa mikoa yote miwili ya Mbeya na Iringa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara hao wanawake masokoni kujiunga na umoja huo kitaifa.

No comments:

Post a Comment

Pages