Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii, Wanamichezo na Waandishi wa habari (Shiwata) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini kesho asubuhi wanatarajia kumsomea dua aliyekuwa Mwenyekiti wa mtandao huo, Taalib Cassim aliyefariki dunia Juni 9 mwaka jana.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Makamu Mwenykiti wa Shiwata, Michael Kagondela alisema dua hiyo ya kumbukizi la mwaka mmoja wa kifo cha marehemu huyo kitasomwa katika Chuo cha Splendid kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam.
Kagondela alisema kisomo hicho kitaongozwa na masheikh mbalimbali wakiwaongoza wadau wengine watakaohudhuria.
"Mwaka huu tunaanza kumsomea aliyekuwa Mwenyekiti wetu ambaye ametangulia mbele ya haki, tunafikiria kutekeleza mambo makubwa zaidi kwani mwenzetu ameanzisha mtandao wa kuwakutanisha wanamichezo, waandishi wa habari na wasanii, hivvyo sisi tunatakiwa kufikiria kutenda makubwa zaidi ya aliyoyafanya mwenzetu," alisema Kagondela.
Aidha Kagondela alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanachama na wadau mbalimbali wanaokumbuka mchango wa mwenyekiti wao kujitokeza kwa wingi katika kisomo hicho.
No comments:
Post a Comment