Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB Makao Makuu, Donatus Richard,
akizungumza na wajasiriamali na wafanyabiashara ambao ni wajumbe wa NMB
Business Club ya mkoani Mwanza, wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo
wajumbe hao. Kushoto ni Mwenyekiti wa Club hiyo anayemaliza muda wake,
Mathiasi Rwechungura na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Godfrey
Mzava.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, akizungumza na
wajasiriamali na wafanyabiashara ambao ni wajumbe wa NMB Business Club
ya mkoani Mwanza, jinsi walivyojipanga kuwalinda watu, mali na biashara
zao wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe hao,kushoto ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava na Mkuu wa kitengo cha
Biashara wa NMB Makao Makuu Donatus Richard. (kulia).
Na Mwandishi Wetu
MKUU
wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Jumanne Murilo amewahakikisha usalama
wa pesa na mali zao.Akizungumza na wafanyabiashara katika Jukwaa la
business club,Jeshi lake limejipanga imara kuhakikisha wanafanyabiashara
hawasumbuliwi na wahalifu.
Aliwaomba
wafanyabiashara mkoani hapa kuhakikisha wanatumia vyema jukwaa la
Business Club katika kuhakikisha wanajenga uchumi imara wa nchi.
'"tumejipanga na tunapambana kuzuia uhalifu kabla haujatokea kuliko kukabiliana nao ukishatokea " Murilo alisema.
Alisema
wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi bali wahakikishe wanafanya biashara
zao kwa uhuru kwakuwa jeshi lake limejipanga vyema kuhakikisha hakuna
masuala ya uhalifu.
Kwa upande wake,mkuu wa kitengo
cha Biashara cha benki ya NMB makao makuu,Donatus Richard alisema benki
yao itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kupitia ‘Business Club’
Alisema
kupitia elimu watakazokuwa wanatoa kwa wafanyabiashara zitakuwa
zikiwasaidia sana wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku.
Donatus
alisema kwa sasa benki yao itaendelea kuwa karibu na wateja wao na
alisema wataendelea kutoa mafunzo mbali mbali kwa wateja wao yakiwemo
masuala ya masoko pamoja na kodi.
Alisema
semina zao pia zimewasaidia wateja wao kuwa karibu na wateja wenzao
ambapo jambo linalodumisha uhusiano mwema katika ufanyaji biashara zao.
Alisema
kwa sasa benki yao ipo katika mikakati ya kuwapeleka wafanyabiashara 10
nchini China kwajili ya kuwenda kujifunza mambo ya kibiashara katika
tamasha la biashara litakalo fanyika nchini humo katika mwezi wa
10, mwaka huu. Mmoja ya wafanyabiashara, Kejja Misungwi, alisema anaiomba
benki ya NMB kuhakiksha wanaendelea kutoa semina za mara kwa mara kwa
wateja wao jambo ambalo litawasaidia wateja kupata elimu za biashara
zitakazowawesha upatakinaji wa faida katika biashara zao.
No comments:
Post a Comment