HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 17, 2019

MITANDAO YA KIJAMII UKUZA BIASHARA

Na Faraja Ezra
IMEELEZWA kuwa moja ya njia ya kukuza biashara nchini ni matumizi ya mitandao ya kijamii katika kusambaza taarifa mbalimbali za kibiashara ili kukuza sekta hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano hoteli hiyo, Lilian Kisasa, amesema ili kukuza sekta ya biashara nchini wameweka mikakati ya kuboresha uchumi wa nchi ili ufanane na nchi zilizoendelea.
Aidha pia kuongeza uelewa kwa wafanya biashara lakini pia kubadilisha mtizamo katika ukuaji wa uchumi nchini katika kuboresha soko la ndani.
Mmoja ya mikakati hiyo ni kutoa hamasa kwa Watanzania kutumia biashara ya kimtandao ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia taifa kwa ujumla.
Pili, alisema kuwaalika wadau wabobezi kutoka nchi mbalimbali duniani kutoa mafunzo ya kibiashara  na kupeana uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto ili kuwanoa wafanyabiashara wazawa.
"Mikakati hiyo imeshaanza kutekelezwa kwa kupokea wakufunzi kutoka Afrika Kusini na Dubai kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara nchini,"alisema Kisasa.
Alisema awamu ya pili ya mafunzo hayo yatafanyika Novemba  mwaka huu katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam huku ikihudhuriwa na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kukuza biashara.
Meneja Kisasa alisema kuwa ili kufikia uchumi wa kati ni lazima Watanzania kuwa wabunifu wa kutumia mitandao ya jamii katika kusambaza taarifa mbalimbali ikiwemo hali ya biashara kwa maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages