Msanii wa Filamu Wema Sepetu akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo baada ya mahakama hiyo kutoa maamuzi ya kwenda Gereza la Segerea kwa siku nane. Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili hivyo mahakama ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.
Msanii
wa Filamu Wema Sepetu akiingia katika gari la magereza.
Wema Sepetu akipaelekea kupanda gari la magereza baada ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa
maamuzi ya kwenda Gereza la Segerea kwa siku nane.
Na Janeth Jovin
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru msanii wa filamu Wema Sepetu kukaa
gerezani kwa siku nane wakati akisubiri maamuzi ya dhamana.
Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili hivyo mahakama ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.
Akitoa
maamuzi hayo leo, Hakimu Mkazi, Maira Kasonde alisema kutokana na
masuala yaliyoletwa mahakamani hapo yanahusu dhamana, atatoa uamuzi.
Alisema kesi hiyo itakuja Juni 24, mwaka huu hivyo mshitakiwa anatakiwa kukaa ndani hadi tarehe hiyo.
Akijitetea
kwanini asifutiwe dhamana, Wema alidai ni kweli hakufika mahakamani
Mei 11 na Juni 14, mwaka huu, ambapo alidai mara ya kwanza alisafiri
kikazi nje ya mkoa ambapo alikwenda mkoani Morogoro na kwamba alimpa
taarifa wakili wake.
Alidai
mara ya pili, alifika mahakamani lakini alishindwa kuingia kwenye
chumba cha mahakama kusikiliza kesi yake kwa sababu aliumwa ghafla tumbo
la hedhi.
Alidai
anapofika tarehe ya hedhi mara nyingi tumbo humuuma hivyo alienda
hospitali kwa ajili ya kuchomwa sindano ya diclopa. Hata hivyo, aliomba
mahakama imsamehe kwa kutokuhudhuria mahakamani.
Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai mshitakiwa hana rekodi yakutohudhuria mahakamani hivyo mahakama impe onyo.
Pia alimtaka mshitakiwa endapo atapata udhuru kuwapa taarifa wadhamini wake ili kuepuka usumbufu kwa mahakama.
Juni
11, mwaka hu upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Sylvia Mitanto
ulidai kwamba mshitakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.
Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.
Wema
anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo
mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono
kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina
maudhui.
No comments:
Post a Comment