HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2019

DC KASESELA MAJANGIRI HAWANA NAFASI KUFANYA UHARIFU KWENYE MBUGA ZA WILAYA YA IRINGA

 Mkuu wa Wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliasili na misitu, Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote na akiwa ameshika silaha bora ambazo wanazitumia walinzi wa hifadhi Village Game Scouts ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS.
 Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu, Richard Kasesela akiwa pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Hashimu Komba  wakiwa kwenye picha moja na viongozi na walinzi wa hifadhi Village Game Scouts.
MKUU wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu iliyopo katika wilaya hiyo.

 NA FREDY MGUNDA, IRINGA

MKUU wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu iliyopo katika wilaya hiyo.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya ghafla ya kuwatembelea na kuwapa moyo walinzi wa hifadhi Village Game Scouts ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS  kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulinda maliasili zilizopo katika wilaya hiyo.

“Mimi niwapongeze sana maana mnafanyakazi kubwa sana kupambana na majangili huko porini jambo ambalo mnapaswa kupongezwa kwa namna yoyote ile” alisema Kasesela
  
Kasesela alisema kuwa hifadhi hizo zimekuwa zikivamiwa na majangili hasa pembezoni mwa hifadhi hizo kutokana na kuwa jirani na wakazi ambao wamekuwa wakifanya uharifu huo kutokana na tamaa zao.

Kasesela aliwaonya majangili kwamba sasa wasirogwe kuingia kwenye mbuga za wanyama kutaka kufanya ujangili wa aina yoyote kwakuwa wanamifumo ya kisasa zikiwemo kamera zimefungwa kwenye maeneo ya mbuga hizo.

“Yoyote atakaye kamatwa kwa ujangili atafikishwa kwenye vyombo husika na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa atakuwa amefanya uharifu ambao haukubariki kisheria” alisema Kasesela

Aidha Kasesela  alilipongeza shirika la STEPS kwa kuwafadhili walinzi wa hifadhi Village Game Scouts kwa kuwapa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo ya ulinzi kwenye mbuga zilizopo katika wilaya ya Iringa.

No comments:

Post a Comment

Pages