HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2019

Membe afunguka Sakata la Lissu kuvuliwa ubunge na utekaji nchini

Na Janeth Jovin

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe (pichani), amesema matukio ya utekaji yanayoendelea kutekea nchini  ni Utamaduni mpya ambao haukubaliki na utaiondolea nchi sifa na heshima iliyonayo duniani.

Akizungumza na waandishi wa nje  ya Mahakama Kuu, Membe, amesema suala hilo pia linaweza kuiondolea usalama nchi na kujenga chuki kubwa kwa wananchi dhidi ya Serikali.

Anasema ni muhimu kwa viongozi wote wa chama, Serikali na wa dini kulikemea jambo hili ili lisiendelee kutekea.

"Huu ni utamaduni mpya ambao haukubaliki na ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba suala la utekaji na watu kupotea linaweza kuiondolea nchi yetu heshima duniani tangu tupate uhuru, hivyo ningependa kuwaomba viongozi wote wa chama na Serikali kulikemea jambo hili,  tuchukue mfano ni mtoto wako ndo amepotea hujui yuko wapi kwa vyovyote vile wenzetu wa dunia hasa watalii watashindwa kuja nchini" amesema Membe.

Anasema kama hali hiyo itaendelea hata wawekezaji wanaowekeza nchini watashindwa kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuhofia usalama.

"Huu ni utamaduni ambao hatukuwa nao huko nje,  viongozi wa serikali na kwenye chama wasione aibu hata wa Dini zote nao wasiogope, wastaafu wote lazima tukemee utamaduni huu mpya, hatuwezi kuendelea kuishi katika nchi yenye watu wenye wasiwasi na uoga ambao hawajui kesho wataamka vipi na hii ajenda iishe maana isipo isha itakwenda mwakani kwenye uchaguzi,"amesema.

Kuhusu Lissu

Kuhusu Mbunge wa Singida Mashariki  Tundu Lissu, Membe alisema hata yeye alimeshangazwa na uamuzi wa Spika wa Bunge Job Ndugai kumvua ubunge Lissu.

Anasema anaamini kuwa Lissu anaweza kupata haki yake ya kuwa Mbunge tena akienda mahakamani.

"Mimi nilishangazwa na uamuzi huo wa Spika sasa tusubiri Lissu arudi aende mahakamani na kama kuna haki basi ataipata huko mahakamani, " alisema

No comments:

Post a Comment

Pages