HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2019

WATAALAMU WATAKIWA KUSHAURI MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA MAENDELEO

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa rais mteule wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania, Profesa Yunus Mgaya Prof. Yunus Mgaya, kabla ya uzinduzi wa baraza hilo.
 Rais wa Baraza la Akademia ya Sayansi Tanzania aliyemaliza muda wake, Prof. Ester Mwaikambo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la tatu la Akademia ya Sayansi Tanzania (TAAS).
Prof. Ester Mwaikambo, akitoa hotuba yake.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, akimpongeza Prof. Ester Mwaikambo kwa hotuba yake.
 Rais mteule wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania, Profesa Yunus Mgaya, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa baraza hilo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, akimpongeza Rais mteule wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania, Profesa Yunus Mgay.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,  akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,  akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,  akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,  akimkabidhi vitendea kazi rais mteule wa Baraza jipya la Akademia ya Sayansi Tanzania.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,  akimkabidhi vitendea kazi rais wa TAAS aliyemaliza muda wake Prof. Ester Mwaikambo.

 
Katibu Mkuu wa TAAS, Prof. Eligius Lyamuya, akipokea vitendeakazi.
Katibu Mkuu wa TAAS, Prof. Eligius Lyamuya, akitoa neno la Shukrani.
Picha ya pamoja.


 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka wanasayansi wanachama wa Akademia ya Sayansi Tanzania (TAAS), kutumia ujuzi wao kutoa ushauri wa matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika shughuli za maendeleo nchini.

Amesema hayo, jijini Dar Es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la tatu la Akademia hiyo ya Sayansi Tanzania lenye wajumbe wanasayansi kutoka nyanja mbalimbali za Sayansi Nchini.

Katika hotuba yake Ndalichako amepongeza mabaraza yaliyotangulia kwa kuendeleza Akademia hiyo iliyoanza rasmi mwaka 2005, ambapo wanachama katika Akademia hiyo wanafanya kazi mbalimbali kwa kujitolea. Aidha amepongeza na kushukuru Baraza la pili lililomaliza muda wake chini ya uongozi wa Prof. Ester Mwaikambo aliekuwa rais wa Akademia kwa juhudi mbalimbali walizofanya katika kukuza taaluma ya Sayansi na wanataaluma.

 “ natambua mchango wa Baraza hili la wanataaluma katika kuhamasisha, kukuza na kuendeleza matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya kitaifa umejidhihirisha wazi”.

Aidha Ndalichako amempongeza rais mteule wa Baraza jipya, Profesa Yunus Mgaya na wajumbe wake kwa kuteuliwa katika nafasi hizo muhimu huku akiwaasa kusimamia vema ushiriki wa Akademia ya Sayansi Tanzania kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Sayansi, Teknolojia na Ubunifu vinatumika kama nyenzo ya kuleta maendeleo endelevu ya uchumi nchini.

“ mpango wa Pili wa Mandeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 unalenga kujenga uchumi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025; Mpango umeeleza bayana kuwa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni nyezo muhimu katika azma hivyo serikali na wataalamu kama ninyi tunawajibu wa kuhamasisha matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika jamii ”.

Aliongezea kuwa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia imechukua hatua mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ikiwa ni pamoja  pamoja na kuboresha miundombinu ya kufundishia katika ngazi zote za elimu, kuzindua Mwongozo wa kutambua na kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa, kuanzisha vituo vya kulea ubunifu na ugunduzi ambapo kwa mwaka 2018/2019 Serikali imewawezesha wabunifu 30 kwa kutoa Shilingi bilioni 1.240 .

Ndalichako pia aliasa Akademia ya Sayansi, kutoa mchango wake katika masuala ya Kukuza na kuendeleza Ubunifu na Ugunduzi wa maarifa ya kisayansi katika nyanja za kijamii na kiuchumi kwa kutoa ushauri na maoni kuhusu Sera na  mikakati ya kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu,  kufanya tafiti za kisayansi zenye kutoa utatuzi wa  changamoto katika jamii hasa kipindi hiki dunia inapoelekea katika mapinduzi ya nne ya viwanda, huku akiahidi Wizara kushirikiana na Akademia.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Ndalichako, rais mteule wa TAAS Prof. Yunus Mgaya amesema academia hiyo yenye wanachama 131 kwa sasa imejipanga kuongeza wanachama na kufanya tafiti, kusaidia wanasayansi kuchapisha tafiti hizo katoika majarida yanayotambulika kimataifa, lakini kubwa zaidi ni kuhuisha matumizi ya Sayansi na teknolojia katika maendeleo ya uchumi.

No comments:

Post a Comment

Pages