Ofisa
Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi,
(kushoto), akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa,
Gulamhafeez Mukadam, ikiwa ni ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT
Taifa unaotarajiwa kuanza leo jijini Mwanza na kufunguliwa na Rais John
Magufuli. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali
NMB, Vicky Bishubo na Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya (wa pili
kulia). NMB ndiye mdhamini mkuu wa mkutano huo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mwenyekiti wa ALAT Taifa - Mh Gulamhafeez Mukadam
akiangalia kwa makini mfano wa hundi ya shilingi Milioni 150
aliyopewa na Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati, Filbert Mponzi
kama ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa
unaotegemewa unaoanza leo jijini Mwanza na kufunguliwa na
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Wanaoangalia
ni Katibu Mkuu wa ALAT , Elirehema Kaaya. NMB ndiye Mdhamini
Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa.
Mwenyekiti wa ALAT Taifa - Mh Gulamhafeez Mukadam
akiondoka kwa mbwembwe na cheki ya mfano ya shilingi Milioni 150
aliyopewa na Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi
kama ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa
unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wanaoangalia
ni Katibu Mkuu wa ALAT - Elirehema Kaaya wa pili na Mjumbe wa Kamati
Tendaji ya ALAT Mh Zaynab Vulu. NMB ndiye Mdhamini
Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Benki ya NMB
imesaidia Zaidi ya shilingi Milioni 150 kwaajili ya Mikutano Mikuu ya Serikali
za Mitaa na Tawala za Mikoa (ALAT) kwa miaka mitano mfululizo huku wakiahidi
kuendelea kushirikiana na serikali za mitaa nchini kutatua changamotoi
mbalimbali.
Afisa Mkuu
wa Wateja Wadogo na wa Kati, Filbert Mponzi aliyasema hayo juzi jijini Mwanza
wakati akikabidhi udhamini wa Benki hiyo kama mdhamini Mkuu wa wa Mkutano Mkuu
wa Mwaka wa ALAT unaoanza leo katika Hoteli ya Malaika Beach jijini Mwanza.
Mponzi
alisema kuwa Benki hiyo inatambua mahusiano ya kibiashara yaliyopo kati ya NMB
na ALAT kupitia Zaidi ya halmashauri 180 ambapo Benki inashiriana kukusanya
mapato ya Serikali huku akisema kusema kuwa taasisi hiyo ni
mmbia wa karibu na serikali, hivyo mahusiano ya NMB na ALAT yameanza muda mrefu
uliopita.
“Tunaishukuru
sekretariet ya Alat pamoja na wajumbe wote kwa kuendelea kutoa ushirikiano,
kufanya biashara pamoja na sisi kama benki tumekuwa tukiendelea kuboresha
huduma zetu ili kuweza kuhudumia serikali kuu pamoja na serikali za mitaa,”
alisema Mponzi.
“Tumepeleka huduma zetu nchi nzima huku
tukizifikia Zaidi ya halmashauri 180 tukiwahudumia katika Nyanja mbalimbali za
kibenki kuanzia wafanyakazi, wafanyabiashara na wajasiliamari na pia madiwani nah ii inaonyesha utayari
wetu wa kuhudumia Serikali za mitaa.” alisema Mponzi.
Mwenyekiti
wa ALAT taifa - Gulamhafeez Mukadam ameishukuru Benki ya NMB kwa kuonyesha
kujali Serikali za mitaa na mchango wa mwaka huu unaonyesha dhamira na
ushirikiano wa kweli kati ya taasisi mbili.
Mheshimiwa Mukadam
aliongeza kuwa jamii za Serikali za mitaa na mamlaka zake bado zinakabiliwa na
changamoto nyingi ambazo zinahitaji kushikwa mkono na taasisi kama NMB kwaajili
ya kusaidiana kutatua changamoto hizo.
Aliiomba pia
Benki ya NMB kuangalia namna ya kuangalia upya misaada yake inayotolewa kwa
jamii kupitia uwajibikaji kwa jamii (CSR) akiomba Benki kuanza kusaidia jambo
ambalo mwisho linakuwa kubwa kuliko misaada midogo midogo ambayo inaweza ikawa
na mchango mdogo kwenye jamii.
Mukadam
alitoa mfano wa misaada ya vifaa vya ujenzi mashuleni na mahospitalini na
kusema kuliko kusaidia vifaa vya kuezekea, ichukue mradi mzima kama ni ujenzi
wa darasa mpaka unakamilika kwa manufaa ya jamii.
“Nafikiria Benki inaweza sasa ikabadiri
muelekeo wake kuhusu misaada mbalimbali kwa jamii, kwa kuhakikisha wanachukua
mradi hata mmoja mkubwa kwenye wilaya na kuhakikisha wanaukamilisha kwa
usimamizi wao ambao utaleta ile thamani halisi ya fedha wanazotoa.” alisema.
Mjumbe wa
Kamati Tendaji ya ALAT na Meya wa Sumbawanga, Justine Malisawa aliishukuru
Benki ya NMB kwa kuleta mfumo wa ukusanyaji mapato ya halmashauri kielektroniki
na kuisifia kuwa imeleta mafanikio makubwa kwa mapato ya Serikali kuongezeka
tofauti na ilivyokuwa zamani hasa ndani ya miaka hii mitatu.
Maneno ya
Bwana Malisawa yaliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu wa Kisarawe na Mjumbe
wa Kamati tendaji ya ALAT – Mh Zaynab Vuli huku akisema Benki hiyo
imejipambanua kwa kufika maeneo ambayo Benki zingine hazijafika.
Mh Vulu
aliiomba Benki hiyo kupunguza riba na kutoa mikopo nafuu kwa wafanya biashara
wadogo hasa wale wanaofanya biashara zao vijijini ili kusaidia maendeleo ya mtu
mmoja mmoja nchini.
No comments:
Post a Comment