Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu akizungumza na Waoneshaji kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii
wa Utamaduni ya Serengeti yanayofanyika wilayani Serengeti mkoani
Mara. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiwa na
pamoja na viongozi wengine. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa tatu kulia) akiwa na Mbunge wa Serengeti, Mhe.Chacha Ryoba ( katikati)
wakipewa maelezo na muuza vinyago ambaye ni miongoni mwa Washiriki wa
Maonesho hayo ya Utalii wa Kiutamaduni huku akiwa ameshika kinyago
alipokuwa akimuelezea ubora wa Kinyago hicho katika Maonesho ya Utalii
wa Utamaduni ya Serengeti yaliyofunguliwa rasmi mkoani Mara. Wa kwanza
kulia ni Mkurugenzi wa Maonesho hayo, Joshua Nyansiri.
Mku wa wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu akizungumza
na Waoneshaji kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya
Serengeti yanayofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu kwa ajili ya kufungua maonesho hayo.
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameiagiza
Hifadhi za Taifa ( TANAPA) kupitia upya sheria ya tozo ya kiingilio kwa
watalii wanapotoka nje ya Hifadhi inayowalazimu kulipwa tena
wanapoingia ndani ya Hifadhi maarufu kwa jina la Single Entry waiondoe
kwenye maeneo yanayolalamikiwa kuwa imeua shughuli za Utalii kwenye
vijiji vinavyozunguka Hifadhi.
Aidha,Mhe.
Kanyasu ameagiza TANAPA iangalie maeneo ambayo inadhani ni muhimu kwa
Single Entry iendelee kutumika kuwa waweke mfumo wa kielektroniki wa
utambuzi wa vidole ( Biometric Identity) utakaoweza kutumika kubaini
udanganyifu endapo utafanyika.
Amesema mfumo huo utawalazimisha watalii kuweka kidole wakati wakiwa wanaingia na wakati wanapotoka nje ya Hifadhi.
Amesema
hali hiyo itawasaidia Waongoza watalii kutoka nje ya Hifadhi na
Watalii wao kwa ajili kuzitembelea jamii zilizokaribu na Hifadhi na
hivyo kuzisaidia jamii kunufaika moja kwa moja kupitia utalii wa
kiutamaduni.
Hayo
yamesemwa kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu wakati alipokuwa akifunga Maonesho ya 8 ya Utalii wa Utamaduni
ya Serengeti mkoani Mara.
Amesema
tangu kuanzishwa kwa Single Entry kumepelekea madhara makubwa kwa
baadhi ya maeneo yaliyo karibu na Hifadhi za Taifa kudumaa kiutalii.
Ameyataja
maeneo hayo yaliyokaribu na yaliyoathirika moja kwa moja kuwa ni ukanda
wa Magharibi katika geti la Ndabaka katika Hifadhi ya Serengeti na
katika Hifadhi ya Ruaha.
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa Maonesho hayo, Kanyasu amesema maeneo yaliyoathirika
zaidi kutokana na kuwepo kwa Single Entry ni yale maeneo ambayo
hayajapitiwa na barabara kuu pamoja na viwanja vya ndege.
Ametaja
sababu zilizopelekea kufa kiutalii maeneo hayo kuwa watalii walio
wengi hulazimika kukaa ndani ya Hifadhi hadi muda wa masaa 24
yanavyoisha bila kutoka wakikwepa gharama endapo watatoka.
Kwa
upande wake, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alimueleza Naibu
Waziri huyo kuwa wilaya yake asilimia 80 ni eneo la Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti hivyo kutokana na uwepo wa Single entry wilaya hivyo
imeathirika sana kwa vile imekosa watalii wanaotembelea vijijini tofauti
na ilivyokuwa mwanzo kabla ya kuanzishwa.
"
Mhe.Waziri tunakuomba uliangalie suala hili, utalii wa kiutamaduni
uliosaidia kuajiri wananchi wengi umekufa kutokana na Single Entry"
alisisitiza
Ameongeza
kuwa endapo itaondolewa itasaidia watalii kuweza kutoka nje ya Hifadhi
kuembelea vituo vingi vya utalii ambavyo vipo nje ya Hifadhi.
Naye,
Anaeli Kilemi aliyesoma risala mbele ya Waziri huyo amesema Single
entry imewadidimiza wananchi wengi ambao walikuwa wamejiajiri kupitia
utalii wa kiutamaduni, Hivyo anaiomba serikali itatue tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment