Mhasibu wa wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bwana Beatrice Kilimo (wapili kushoto),
akitoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira kwa mwananchi (kulia)
aliyetembelea banda la baraza hilo katika maonesho ya 43 ya biashara ya
kimataifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mazingira Mwandamizi wa
NEMC, Bi. Pendo Kundya.
Mkaguzi
wa Mazingira wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC), Bwana Nelson Nyabise (kulia) akitoa elimu juu ya utunzaji wa
mazingira kwa mwananchi aliyetembelea banda la baraza hilo katika
Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeendelea kutoa elimu kwa wananchi
juu ya utunzaji wa mazingira, kutoa huduma za ulipaji watozo za tathmini ya
athari kwa mazingira (EIA), Ukaguzi wa mazingira (EA) pamoja na masuala mbalimbali
yanayohusu mazingira.
NEMC
imeshiriki katika maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa maarufu sabasaba
wakishiriki katika Banda la Katavi chumba namba 53 na 54 kwa madhumuni ya
kuuhabarisha umma juu ya majukumu yake katika swala la mazingira.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana katika maonesho hayo yanayoendelea jijini Dar es
Salaam, Afisa Mazingira Mwandamizi wa NEMC, Bi. Pendo Kundya alisema kuwa
dhumuni la NEMC kuwepo katika viwanja hivyo ni kutoa elimu ili kujenga uelewa
mpana kwa wananchi juu ya umuhimu utunzaji mazingira.
“Mudhumini letu ni
kuendelea kuuhabarisha umma juu ya utunzaji wa mazingira na pia kuhamasisha juu
ya katazo la Serikali la matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko mbadala
iliyothibishwa na mamlaka husika kutumiwa na jamii,” alisema
Aidha Bi Kundya
aliongeza kuwa mazingira ni muhimu yakatunzwa ili athari zitokanazo na
uharibifu wa mazingira usituathiri kama nchini kwa kujijengea mazoea ya kufanya
usafi katika mazingira yanayotuzunguka.
“Katika banda hilo
NEMC wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo kupokea tozo za EIA pamoja na EA kwa
mwaka 2019//2020 kwa wadau ambao hawajalipa,”Bi.Kundya alisema.
Alisema Baraza
liimesogeza huduma za malipo ya tozo za EIA na EA ili wadau wa mazingira waweze kuzilipia hapa kwani katika maonesho
haya wadau wengi hujitokeza ili kupata maelezo ya mambo mbalimbali yanayofanywa
na kampuni au taasisi mbalimbali za ndani nan je ya nchi.
Kwa upande wake
Mkaguzi wa Mazingira wa NEMC Bwana Nelson Nyabise alisema NEMC wanaendelea kutoa elimu na mwongozo kwa
wadau wa mazingira ambao hufanya shughuli za ukusanyaji,utunzaji na
usafirishaji wa taka hatarishi kama betri chakavu, taka za
kieletronic na oil chafu ili zisiweze kuleta madhara kwa wananchi.
“Athari za taka
hatarishi ni hatari kwa ustawi wa mazingira hivyo katika banda letu tunaendelea
kutoa elimu kuhusu namna nzuri ya kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka
hatarishi ili zisilete madhara kwa wananchi,’ alisema Bw. Nyabise
Naye Afisa Mazingira
wa NEMC, Bwana Elias Chundu alipongeza mwitikio wa watanzania katika kufuatilia
masuala mbalimbali yanayohusu mazingira huku wengine wakitoa maoni ambayo Baraza
imeahidi kuyafanyia kazi
“Kumekuwa na mwitikio
mkubwa kwa watanzania katika kufuatilia masuala yanayohusu mazingira na hasa
mkikumbuka hivi karibuni kulikuwa na marufuku ya utumiaji wa mifuko ya plastiki
ambapo walitii marufuku hiyo pasipo kutumia nguvu,” alisema Bw.
Chundu.
Wananchi kadhaa
waliotembelea banda hilo walitoa pongezi kwa Baraza hilo katika kusimamia
sheria na kanuni za mazingira na kutoa wito kuendelea kutoa elimu kupitia
vyombo vya habari juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
“NEMC inafanya kazi
nzuri kuhakikisha elimu ya utunzaji wa mazingira inawafikia mwananchi wote na
nimefurahi kuwakuta katika maonesho haya, hii inaonyesha ni namna gani
wamejipanga katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya mazingira,” alisema Bi Mary
Joshua.alipotembelea banda la NEMC.
Alisema zipo baadhi ya
changamoto wanazotakiwa kuzifanyia kazi kama NEMC ikiwa ni pamoja na
tatizo la kelele zinazotoka katika baa, kumbi za starehe na ibada za mikesha
ambapo zinawaathiri wananchi wengi.
NEMC wameendelea
kuungwa mkono na wananchi na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa hatua
wanazochukua ikiwemo upigaji marufuku wa matumizi ya mifuko ya plastiki.
No comments:
Post a Comment