Na Tatu Mohamed
KATIKA
kuendana na soko la ushindani, Shirika la Posta Tanzania, limeanzisha
duka jipya la biashara za kimtandao maarufu kama 'Posta Shop Tz'.
Akizungumza na Habari Mseto leo Julai 2, 2019 katika viwanja vya maonesho
ya 43 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam (DITF) yanayofanyika
katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Meneja wa Biashara za
kielekroniki(E-commerce), Amina Salum (pichani), amesema ni duka ambalo linauwezo
wa kuuza, kununua na kutangaza biashara kwa wateja ambao wamejisajili.
"Mjasiliamali yeyote anaweza kujiunga kupitia website yetu ya www.postashoptz au kuingia kwenye website ya shirika ya www.posta.co.tz," amesema.
Amesema wameamua kuanzisha hivyo kwasababu biashara za kimtandao kwasasa zinauzika sana.
"Vijana
wengi sasa hivi wananunua bidhaa online, kwa kuwa shirika linafanya
biashara na linaaminika zaidi hivyo tukaona na sisi tuje na duka hili
ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga nasi bure kabisa " amesema Amina.
Hata
hivyo aliongeza kuwa muamko umekuwa mkubwa kwa watanzania kutembelea
banda lao na kutaka kujifunza mambo mbalimbali ya shirika hilo.
Ameongeza
kuwa shirika hilo wamejipanga kama ambavyo kampuni zingine zimejipanga
na wanafanya kazi na kampuni zote za simu nchini.
No comments:
Post a Comment