Mkurugenzi wa Chemchem Nicolas Negri akipokea zawadi kutoka kwa akina mama wa jamii ya kibarbeig kutokana na kuwezeshwa vikundi vyao.
Wanawake wa jamii ya kibarbeig wakiwa kwenye kikao cha vikoba baada ya kupatiwa mkopo na Taasisi ya Chemchem.
Mwandishi Wetu, Babati
WAFUGAJI jamii ya Kibarbeig wilayani Babati, mkoa wa Manyara wanatarajiwa kuanza kunufaika zaidi na Utalii baada ya kuanzishwa vituo vya kuvutia watalii katika maeneo yao.
Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya Chemchem association, Walter Palangyo amesema,Taasisi hiyo iliyowekeza shughuli za Utalii,katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, kupitia hoteli za Kitalii za Chemchem imejipanga kuboresha maisha ya jamii hiyo ili inufaike zaidi na Utalii.
Anasema jamii hii iliyopo katika kijiji cha Vilima vitatu, imewezeshwa kupitia vikundi vyao vya Vikoba na itajengewa maboma ya kitalii ambayo yatakuwa yakitembelewa na watalii ambayo watalipa fedha.
"kuna kikundi cha Wicheda ba na Datoga vya jamii ya kibarbeig ambavyo tumepatia kiasi cha sh 2.5 milioni ili kukuza mitaji yao na kuweza kufanya shughuli za kijasiriamali ikiwepo kuuza vitu vya asili kwa watalii "anasema
Kamishna wa uhifadhi wa Mamlaka ya wanyamapori (TAWA), Dk James Wakibara anasema jamii zilizopo eneo hilo la hifadhi ya jamii,linaweza kunufaika sana na Utalii kama wakizitumia fursa zilizopo.
" mwaka jana hifadhi hii imeingiza zaidi ya sh 1.2 bilion hivyo mnaweza kunufaika zaidi kama mkiendelea kuhifadhi eneo hili na kutumia fursa zavutalii zilizopo"amesema.
No comments:
Post a Comment