Meneja WMA Pwani, Alban Kihulla, akizungumza na waandishi wa habari
walipotembela katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu sabasaba yanayoendelea
kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam
Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam
KATIKA
kuendelea kuisapoti serikali katika sekta ya madini, Wakala wa Vipimo
(WMA) imesema tayari imehakiki mizani inayotumika kupimia Madini na Vito
vya thamani na migodini nchi nzima.
Hayo yamebainishwa na Meneja WMA Pwani, Alban Kihulla alipokuwa akizungumza na Habari Mseto katika
banda lao lililopo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa Dar
es Salaam (DITF) maarufu sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya
mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Amesema
uhakiki huo ni miongoni mwa kuisaidia serikali katika sekta ya madini
ili kusaidia mnunuaji kupata kiasi kamili anachokihitaji.
"Wakala
wa vipimo inahakiki mizani inayotumika kununulia madini na vito vya
thamani na migodini, katika masoko ya kuuzia madini na kwa wauzaji wa
madini(sonara). Pia tunatoa ushauri wa kitaalamu kwa Wizara inayohusika
na madini mara kwa mara inapohitajika.
"Kwa
Tanzania bara hakuna mzani usiohakikiwa katika upimaji wa madini kwani
WMA tuna vifaa maalum vya kupimia mizani hiyo," amesema.
Amesema
hiyo inasaidia hata kwa wachimbaji wadogo wanaouza madini katika vituo
mbalimbali nchini kuuza kitu kamili ambacho yeye hawezi kupata hasara
wala mteja kwa sababu kimepimwa katika mzani uliohakikiwa.
Aidha,
Kihulla amesema tayari WMA imekagua dira za maji zipatazo 57000 kwa
kipindi cha Februali mwaka huu na kukuta dira 500 hazipo sawa katika
usomaji wa maji.
Ameongeza
kuwa, mwaka huu katika maonyesho hayo wamekuja na bidhaa mbili za
kuonyesha ikiwemo Dira ya maji pamoja na mizani ya kupimia Vito.
No comments:
Post a Comment