Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo,
wakati alipofungua kituo cha huduma za utalii, katika Wilaya ya Karatu, mkoani
Arusha, Julai 21.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mke wa Bwana Joseph Erro, Bibi Evalina Madawe, ambaye amejitolea kiwanja kilichotumika kujengea kituo cha huduma za
utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni mtoto wa
bwana Francis Theodosia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akipewa maelezo na Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe,
ndani ya kituo kidogo cha Polisi, kilichopo katika kituo cha huduma za utalii wilayani
Karatu, Julai 21.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia
Mahongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kituo
cha huduma za utalii, wilayani Karatu, kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha huduma za utalii, kilichopo katika
Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika
Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika
Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua gari jipya la Polisi, lililokabidhiwa kwa ajili
ya kuwahudumia watalii, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai
21.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi gari jipya la Polisi, litakalotumika kwa ajili
ya kuhudumia watalii, kwa Kaimu RPC Mkoa wa Arusha James Manyara, kwenye kituo
cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua rasmi kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika
Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay,
wilayani Karatu watumie fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha
maisha yao.
“Tumieni fursa ya uwepo wa eneo hili.
Halmashauri wakishajenga vizimba vya biashara, leteni bidhaa zenu kama vile
picha za tingatinga, mapambo, vinyago na vyakula vya asili ili watalii wakija
hapa wapate huduma kutoka kwenu,” alisema.
Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili,
Julai 21, 2019) wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya
kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani na kukabidhi gari la
polisi kwa ajili ya patrol ya watalii
katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha.
Waziri Mkuu alizindua
kituo cha kutolea huduma za usalama kwa watalii wilayani Karatu ikiwa ni ishara
ya kuwakilisha vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha
katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido).
Waziri Mkuu alitumia
fursa hiyo kuwasihi wakazi hao wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya
Tanzania pindi wakirudi makwao. “Ili kukuza na kutangaza utalii, tunapaswa tuwe
na mapenzi mema kwa watalii lakini kikubwa zaidi ni usalama wao.”
Aliwataka wakazi hao
waendelee kuiamini Serikali ya awamu ya tano na waendelee kumuombea Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ili apate nguvu ya kuleta maendeleo zaidi.
Pia aliwashukuru
viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) kwa kuchangia ujenzi
wa vituo hivyo na kutoa gari jipya la polisi kwa ajili kituo hicho cha Karatu.
Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililogharimu
dola za Marekani 45,000, limepewa namba za usajili za PT 4190.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza
na wakazi wa Bashay waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw.
Mrisho Gambo alisema ujenzi wa vituo hivyo umetokana na malalamiko aliyopokea
kwamba watalii wakitoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi kufika Karatu
wanakuwa wamesimamishwa njiani zaidi ya mara 20.
“Tulijiuliza hawa watalii wamekuja kutalii, wanataka
kupumzika, sasa ni kwa nini wasumbuliwe kiasi hicho? Tuliamua kuanzisha vituo
vya aina hii, ili watalii wafanyiwe ukaguzi kwenye check-points maalum,” alisema.
Aliomba Jeshi la Polisi liwapange barabarani askari ambao
ni weledi na wana uelewa wa masuala ya utalii na kutolea mfano wa wiki iliyopita
ambapo alikuwa akitokea mjini kwenda Karatu na kukuta magari ya watalii zaidi
ya 10 yamesimamishwa njiani.
“Niliona baadhi yao wakiwa wamelala kwenye magari kwa
uchovu, nilipowauliza wamekalishwa kwa muda gani, walisema ni kwa zaidi ya
dakika 45. Nilipomuuliza askari aliyewasimamisha ni kwa nini anafanya hivyo,
akanijibu kwamba dereva amemjibu vibaya. Hivi ni kwa nini watalii wateseke
juani wakati mwenye makosa ni dreva?”
Naye, Makamu Mwenyekiti wa TATO, Bw. Henry
Kimaro aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya za kupambana na ujangili na
kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. “Tumeona hivi karibuni watalii
wengine kutoka Israel, China na sasa ndege yetu imeanza kwenda India kuwafuata
hukohuko,” alisema.
Alisema wameanza na vituo hivyo vinne mkoani Arusha lakini
tatizo hilo liko maeneo mengi nchini na wao hawawezi kufika nchi nzima kutoa
huduma kama hiyo. Hivyo, alimuomba Waziri Mkuu awahimize Wakuu wa Wilaya ambao
wilaya zao zinajihusisha na sekta ya utalii, waige mfano wa wilaya ya Karatu
ili kuhakikisha usalama wa watalii wawapo nchini.
No comments:
Post a Comment